30 March 2012

Ujerumani kuboresha huduma ya maji jijini

Na Semeni Masoud
WATAALAMU wa maji kutoka nchini Uj e r uma n i kwa k u s h i r i k i a n a n a Mamlaka ya Maji safi na Maji taka nchini (DAWASCO) wameandaa mpango mkakati wa maji na kikosi cha zima moto ili kuboresha huduma hiyo kwa watumiaji.
Ha y o y a l i b a i n i s hwa n a
Mwakilishi wa Meya wa Jiji la Dar
es Salaam, Bw. Philipo Mwakyusa,
alipokuwa akizungumza juu ya
mpango mkakati wa kuboresha
mamlaka hiyo.
Alisema kuwa moja ya mpango
wa mamlaka hiyo ni kukuza na
kuendeleza miundo mbinu ya
mamlaka hiyo ili iweze kuleta
tija kwa vizazi vya sasa na vizazi
vijavyo.
“Moja ya mpango mkakati wetu
ni kuhakikisha wananchi wetu
wanapata maji safi na yaliyo saf,
hivyo basi tumedhamiria kufanya
hivi kwa kuhakikisha tunaiboresha
miundombinu ya mamlaka yetu
ili iwe changamoto kwao katika
kusambaza maji,” alisema Bw
Mwakyusa.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Jiji la Hamburg Bw. Axel Hinrichs,
alishukuru Tanzania kwa kuonesha
ushirikiano wa baina ya Tanzania
na Ujerumani kwenye shughuli
mbalimbali za kimaendeleo.
Alisema kuwa jiji hilo lipo tayari
kuhakikisha huduma ya maji safi
na salama inapatikana na kuongeza
kuwa Serikali ya Ujerumani
ipo tayari kutoa ushirikiano
wakuboresha miundo mbinu.
“Serikali ya Ujerumani ipo
tayari kushirikiana na Tanzania
kwenye shughuli mbalimbali za
kimaendeleo hususani maji kwa
sababu tunaamini maji ni uhai,”
alisema Bw. Hinrichs.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Huduma za Maji Mijini wa
DAWASA Bi. Mary Mboye, alisema
mradi huo umekuja wakati muafaka
wakati Jiji linakabiliwa na uhaba
wa maji kutokana na uchakavu wa
miundo mbinu inayosafirisha maji.
Alisema kuwa mradi huo
umegharimu kiasi cha shilingi bilioni
miambili na unatarajia kukamilika
baada ya miaka mitatu.

1 comment:

  1. KWA UFISADI HUU, WAJERUMANI MTAFIKA? WENZENU WACHINA WALIJITAHIDI. CHUNGUZENI MATOKEO YAKE. MTAPATA SOMO. HII NI TANZANIA NA DAR ES SALAAM YETU BWANA! LABDA WAJE WAINGEREZA waliotuwekea mfumo wa maji hapo nyuma.

    ReplyDelete