30 March 2012

Ukosefu wa elimu chanzo cha mauaji kwa imani za kishirikina

Wananchi wanatakiwa kuelimishwa kupitia mikutano ya hadhara kuheshimu haki za wenzao ili kukomesha mauaji.


KATIKA miaka ya hivi karibuni kumeibuka wimbi la mauaji yanayohusisha imani za kishirikina. Mauaji hayo hufanywa na wananchi wa eneo husika kupitia mikutano ambapo kwa kutumia silaha za jadi huamua kuwaua watuhumiwa na kuharibu mali zao.

Baadhi ya mauaji haya
huelekezwa katika tuhuma za
uchawi na ujambazi ambapo
jamii kwa makusudi hujichukulia
sheria mikononi bila kuhusisha
vyombo vya dola.
B a a d h i y a v i k o n gwe
wamepoteza maisha na mali
zao kutokana na jamii ya mahali
husika kuwatuhumu kuwa
wanajihusisha na vitendo vya
kishirikina.
Watu wengine wamesingiziwa
kuwa ni majambazi na kuuawa
na kuharibiwa mali zao bila
kufikisha tuhuma hizo katika
vyombo vya usalama.
Wa l ema v u w a n g o z i
(ALBINO) nao wamepoteza
maisha yao kwa imani za
kishirikina kwa madai kuwa
viungo vyao ni bidhaa zenye
thamani kubwa.
Tofauti na mauaji ya vikongwe
wanaotuhumiwa kuwa ni
wachawi, albino wanauawa kwa
siri lakini kwa lengo lile moja ya
kupata utajiri.
Miaka ya hivi karibuni katika
mikoa ya Kanda ya Ziwa vitendo
hivyo viliripotiwa kwa kiwango
kikubwa hadi serikali ilipokemea
kwa nguvu zaidi.
Katika dhana ya mauaji ya
vikongwe kwa sehemu kubwa
inahusisha vikongwe wajane
ambao waume zao walikufa na
kuwaachia urithi wao na watoto
wao.
Mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa
Shinyanga, Mwanza na Mara
kwa sehemu zipo desturi za
baadhi ya makabila kuoa wake
wengi.
Wazee wa familia wanapokufa
huacha urithi wa mashamba na
mali chini ya usimamizi wa wake
zao, hivyo ndugu wa kiume wa
marehemu huwa hawafurahishwi
na kitendo hicho kutokana na
itikadi ya mfumo dume kwamba
ni mwanaume tu ndiye mwenye
mamlaka ya kuhodhi mali na
kuwa na sauti katika familia.
Lakini pia wivu wa mali
hutokana na misingi ya wake
wenza hasa pale ambapo
nyumba ya mwanamke fulani
inapoonekana kufanikiwa kuliko
wengine.
Jambo hili husababisha chuki,
wivu na fi tina miongoni mwa
ndugu wa marehemu na wajane
hao kufaidi urithi wa ndugu
yao.
Hapo ndipo zinapoanza
tuhuma za uchawi na ushirikina
kwa wajane lengo likiwa ni
kuwaondoa ili wao wabaki na
mali hizo.
Baadhi ya wajane hao
huhukumiwa na sura zao
zilizokunjamana kutokana na
uzee na uwekundu wa macho
kuwa ni vigezo vya kujihusisha
na vitendo vya kishirikina.
Hakuna uthibitisho kuwa,
rangi ya macho huashiria uchawi
au mtu kujihusisha na ushirikina
badala yake ni dhana ambayo
inachomekwa ili wanaotuhumu
wapate kibali cha kuharibu
maisha au mali ya mhusika.
Ni watu wangapi wenye sura
nzuri na watanashati, wakiwemo
baadhi ya matajiri na wanasiasa
maarufu lakini ni washirikina
wakubwa wanaokesha makaburini
ili mambo yao yaende vizuri.
Wao hawapigiwi yowe wala
hawachukuliwi sheria mkononi
lakini tuhuma nyingi zinarushwa
kwa wanyonge kwa sababu ya
kile kidogo walichonacho.
Tuhuma hizo huenezwa ndani
ya jamii kiasi cha kuanzisha
vikao vya mijadala, isitoshe
hata baadhi ya serikali ya vijiji
na mitaa uhusishwa na baadhi
kubariki vitendo hivyo vya
ukandamizaji.
Watu hao wenye nia mbaya
hulichukua jeshi la polisi na
hata kulihusisha na kukumbatia
watuhumiwa pale jeshi hilo
linapotaka uthibitisho ili litoe
uamuzi sahihi.
Jamii huamua kuchukua sheria
mkononi kuwaua, kuzichoma
nyumba na kuharibu mali za
mtuhumiwa au kugawana mali
hizo miongoni mwao.
Kwa baadhi ya serikali ya vijiji
ambazo hubarikia maamuzi hayo
mara nyingi mali za watuhumiwa
hudaiwa kutaifishwa na kuwa
mali ya serikali ya kijiji.
Mifano hiyo tunaweza
kushuhudia katika vurugu
iliyofanyika mapema mwaka huu
katika Kijiji cha Kiabakari wilaya
ya Musoma vijijini ambapo baadhi
ya watu kutuhumiwa kujihusisha
na vitendo vya kishirikina na
ujambazi ambapo walitishiwa
kuuawa na kufukuzwa katika
kijiji hicho.
Nyumba zao zilichomwa
moto na mifugo yao zaidi ya
40 na mashamba kutaifishwa
kwa madai kuwa zinawekwa
katika mfuko wa serikali ya
kijiji kuchangia maendeleo ya
kijiji hicho.
Masuala haya yanapaswa
kupingwa vikali na kulaaniwa
popote pale yanapotendeka kwa
kuwa ni kinyume na haki za
binadamu na katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Katiba ya nchi inasema kila
mtu ana haki ya kuishi na kupata
hifadhi ndani ya nchi yake yeye
na mali zake.
Serikali za vijiji, wanasiasa
na viongozi wa dini hawana
budi kuwaelimisha wananchi
vijijini kuhusu uvunjifu wa haki
za wajane hawa ambao hawana
hatia.
Isitoshe kutokana na uchu wa
kupata mali na utajiri baadhi ya
vijana wamekuwa wakiwafanyia
wajane hawa vitendo vya ajabu
ikiwa ni pamoja na kuwabaka,
kuwaua huku jamii ikitafsiri
kuwa vitendo hivyo vinatokana
na imani ya kishirikina.
Dhana hiyo potofu ndiyo
iliyofanya ndugu zetu walemavu
wa ngozi kuingia katika matatizo
ya kuuawa.
Utafi ti unaonesha kuwa, imani
hii ya kupata mali kutokana
na viungo vya albino kwa njia
ya ushirikina ni dhana potofu
iliyojikita ndani ya jamii.
Katika baadhi ya makabila
nchini ni nadra sana kukuta jamii
ya albino kutokana tu kwamba ni
wachache katika jamii hiyo.
Lakini pia baadhi ya jamii
imekuwa ikiwaua walemavu
hao mapema sana mara tu
wanapozaliwa kwa kudai kuwa
wanaondoa mikosi ndani ya
jamii yao.
Wakati wengine wakiwaua
utotoni baadhi huwafanyia kafara
ili kubariki mali na kuondoa
mikosi ndani ya familia husika.
Vitendo hivyo huweza
kuthibitishwa katika baadhi ya
makabila hapa nchini ambapo
kabla ya kuimarika kwa vyombo
vya habari jamii ya albino
walikuwa wakipotea katika
mazingira ya kutatanisha .
Kupotea huko kwa albino
miongoni mwa baadhi ya jamii
inaelezwa kuwa ni kutokana na
viapo vya siri kati ya wazazi
wenyewe na watu walioaminiwa
kuwa wanaweza kufanya
matambiko kutumia viungo vyao
katika kubariki familia husika.
Ni baadhi ya watu waliowahi
kujihusisha katika vitendo hivi
ndio wanaoeneza dhana potofu
hasa wakati huu wa utandawazi
na kuimarika kwa vyombo vya
habari.
Dhana hii ya kutaka kupata
mali kwa njia isiyo halali huku
baadhi ya waliopata mali kwa
juhudi zao wakionewa kijicho
na kusingiziwa ujambazi na
ushirikina imelemaza jamii
yetu.
Si vyema kujenga jamii yenye
mawazo kuwa upatikanaji wa
mali hutokana na ushirikina,
ujambazi na ufi sadi na kwamba
hakuna njia nyingine halali
ambayo mtu anaweza kupata
mali.
Utakuta katika vijiji vyetu
baadhi ya jamii inawaangalia
kwa jicho baya wale waliopata
bahati ya kubarikiwa kupata mali
na kila mara wanapanga mbinu
ya kuwarudisha nyuma ili wote
wawe sawa.
Nalipongeza jeshi la polisi
kuleta mbinu nzuri ya ulinzi
shirikishi ndani ya jamii lakini pia
ina madhara yake pale ambapo
jamii wa eneo husika inapotaka
kumtendea mtu hiana.
Na hapo ndipo dhana ya wengi
wape inapokuwa na kasoro katika
kufanya maamuzi kinyume hasa
katika wakati huu ambapo watu
wengi wanapenda fedha chafu.
Katika zama hizi za ustaarabu ni
vyema serikali, viongozi wa dini
na wadau wengine wa maendeleo
waongeze bidii katika elimu ya
kazi iletayo tija miongoni mwa
jamii.
Mitaala mashuleni kuanzia
shule za misingi, kanuni bora ya
kilimo, biashara na utendaji wa
kazi ingefundishwa ili kujenga
jamii inayoheshimu kazi na
kuamini kuwa mali inapatikana
kwa kufanya kazi kwa bidii.
Hakuna anayeweza kupata
utajiri kwa kuonea kijicho na
wivu mali ya mwenzake kinyume
chake kutazaa chuki, fitina na
uhasama miongoni mwa jamii.
Wapo baadhi ya watu waliowahi
kupata mali lakini kutokana na
kijicho kwa dhana ya ushirikina
watu hawa wamefanywa maskini
kwa mali zao kuharibiwa.
Wa k o w a j a n e w e n g i
wamefanyiwa vitendo vya hiani
katika jamii yetu kutokana na
dhana hii ya ushirikina ambapo
katika maeneo ya mijini nguvu
za pesa na sheria hutumika
kuwadhulumu.
Elimu itasaidia kupunguza
ma t a t i z o h a y a amb a y o
yametawala vijijini kutokana na
wananchi wengi kuikosa

2 comments:

  1. kWELI KABISA ULIYONENE.LAKINI MFANO MWIZI KIZIBITI KIPO,MTU ANAPELEKWA POLISI,BAADA YA MUDA MFUPI ANARUDI KISA KATOA PESA.UTASUBIREI HUENDA ATAITWA MAHAKAMANI LAKINI WAPI.SI HIVYO TU HATA MAHAKAMANI HAKUNA USALAMA KABISA.HAKIMU AKIPEWA MRUNGULA KESI ANAIPINDISHA VIPENGELE KIBAO HATIMAE KESI HAINA USHAIDI.HII SI MANENO TU UDHURIA KESI UONE.HIVYO JESHI LETU LA POLISI NA MAHAKAMA BADO SI SALAMA.NDO MAANA WATU WANAMALIZA ISSUE HAPO KWA PAPO.MFANO KUNA MTU NI JAMBAZI TENA SI KIBAKA.PICHA ZAKE ZIPO VITUO VYA POLISI NA POLISI WANAMUONA KILA SIKU HAWAMKAMATI,SASA HICHO NI NINI.AU NI SAWA NA WAKATI WA NJAA,FAMILIA IMEKOSA CHAKULA CHA JIONI UNACHEMSHA MAJI HADI WATOTO WANALALA,ILI MRADI TU WALALE WASIKUSUMBUE.ANGALIA NCHI AMBAZO WIZI HAUPO KAMA KULE UARABUNI,HAKUNA WIZI WIZI WA MIFUKONI.AU MAJUMBANI USIKU.MAANA TOKA AWALI WALITILIA MKAZO MTU AKIIBA ANAUWAWA.TOKA HAPO WATU WALIOGOPA.SASA HAPA KWETU MTU ANAIBA EVIDENCE ZIPO,ANAFIKISHWA KITUONI BAADA YA MUDA YUKO MTAANI,NDO NINI.SHERIA ZA NCHI ZETU NA WATENDAJI NI DAGANYA TOTO.TUWE WAKALI.

    ReplyDelete
  2. Nimeisoma habari hii kuhusu ukosefu wa elimu na mauaji ya vikongwe na majambazi. Nafikiri mhandishi hajafanya utafiti wa kutosha kuhusu makala yake. Ingawa nakubaliana naye kuhusu mauaji ya albino kwa imani ya kutumia viungo vyao kutafuta mali na kwamba hii ni imani mbovu na isiyokuwa na ukweli wowote, sikubaliani naye kuhusu mauaji yanayohusiana na ushirikina. Mimi ni msomi kwa viwango vyovyote vile, nimekuwa nikipinga imani za kishirikina kwa muda mrefu mpaka niliposhuhudia kwa macho yangu yale yanayofanywa na washirikina. Kuanzia hapo mawazo yangu yamebadilika na uelewa wangu kuwahusu washirikina na ushirikina umebadilika. Ushirikina hupo na madhara yake ni makubwa na mabaya mno. Kama unataka ushahidi wa niliyoyashuhudia nitafute kwa ming2o@yahoo.co.uk

    ReplyDelete