30 March 2012

SIFACU washauri Serikali kuvitazama vyama nchini

Na Damiano Mkumbo, Singida
SE R I K A L I m k o a n i Singida imeshauriwa kuvikutanisha vyama vya ushirika vya msingi na wafanyabiashara waunuzi wa zao la alizeti ili kuwekeana mipaka ya ununuzi wa zao hilo katika kuimarisha mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani.

Ushauri huo ulitolewa na Mjumbe
Mwakilishi wa Chama Kikuu cha
Ushirika mkoani humo (SIFACU),
Bw. Ramadhani Kurwa
juzi mjini Singida alipokuwa
akizungumzia kuhusu kuendeleza
zao hilo kwa lengo la kuwapatia
faida zaidi wakulima.
Bw. Kurwa alieleza kuwa ni
vema vyama hivyo vya msingi
vihusike katika kukusanya alizeti
kutoka kwa wakulima na kuhifadhi
ghalani ili wafanyabiashara binafsi
waweze kununua kulingana na bei
inayomnufaisha mkulima.
Pameanza kujitokeza changamoto
zinazoweza kushusha bei ya zao
hilo ambalo ni mkombozi mkubwa
wa wananchi wa Mkoa wa Singida
ambalo linategemewa katika
uchumi wao hiyo inayotokana na
baadhi ya wafanyabiashara kwenda
moja kwa moja kwa wakulima na
kununua kwa bei ndogo,alisema.
Alibainisha kuwa, hali hiyo
alipowatembelea wakulima
ilionesha kuwa wafanyabiashara
b i n a f s i w a n a w a s h a w i s h i
wakulima kuuza mazao yao
yakiwa ghalani jambo ambalo
linaweza kuwarudisha katika hali
ya umaskini.
Kuna umuhimu kwa Serikali
kuwakutanisha pande hizo mbili
kwa lengo la kuweka msimamo
na mipaka ya utaratibu mzuri
wa ununuzi wa mazao kupitia
mfumo huo rasmi uliyoanza kuleta
mafanikio makubwa kwa wakulima
wa alizeti," alisema.
Alieleza kuwa, mfumo
w a s t a k a b d h i y a m a z a o
ghalani uliyoanza mwaka juzi
umewanufaisha wakulima kwani
zao la alizeti lilipanda bei kutoka
sh. 350 kwa kilo hadi kufikia sh.
730 kwa kilo na kujipatia faida
kubwa.
Kutokana na faida hiyo wakulima
vijijini wamefanikiwa kujenga
nyumba bora za kisasa, kujikimu,
kununua zana bora na kuwa na
uwezo wa kupata vifaa vya usafiri
na mawasiliano na hivyo maisha
yao kuwa mazuri," alisema.

No comments:

Post a Comment