30 March 2012

Kamati ya Mrema yamkaanga DED

Anneth Kagenda na
Flora Amon
 MKURUGENZ I wa Halmashauri ya Magu, Bw. Cornel Ngudungi, ametimuliwa kwenye kikao cha Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), baada ya kutoridhishwa na ripoti yake ya hesabu na imeagiza akatwe asilimia 15 ya mshahara wake ujao.

Mkurugenzi huyo alikumbwa na
maswaibu hayo Dar es Salaam jana
wakati alipowalisisha ripoti yake
kwenye kamati ya LAAT kuhusu
matumizi ya fedha zilizotengwa
kwa ajili ya miradi ya maendeleo
kwenye halmashauri yake.
Akizungumza na waandishi wa
habari Mwenyekiti wa LAAT, Bw.
Augustino Mrema, alisema Kamati
yake imefikia hatua hiyo kutokana
na kutoridhishwa na utendaji wa
Bw. Ngudungi, hivyo ilimpa
mwezi mmoja kuwa amekamilisha
ripoti kwa usahihi.
Alisema onyo hilo kwa
mkurugenzi huyo ni la kwanza hivyo
baada ya kukatwa mshahara wake
atatakiwa kupeleka stakabadhi hizo
kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) ili ripoti zake
zihakikiwe. Pia kamati hiyo iliagiza
aandikiwe barua ya onyo na mwajiri
wake ambaye ni TAMISEMI ili
aache uzembe.
Kwa mujibu wa Bw. Mrema
kamati yake imeagiza wakuu wa
idara nao wakatwe asilimia 15 ya
mshahara wao na kupewa barua za
onyo ili kuwa fundisho.
Alisema wakati mwingine
wakionekana wamefuja fedha za
Serikali kwa uzembe watazilipa
kutoka mifukoni mwao ili
kuimarisha utendaji kazi.
Katika hatua nyingine Bw. Mrema
alisema kamati yake imeipa wiki
mbili Halmashauri ya Wilaya ya
Kwimba kupitia mradi wake wa
afya ( Basketi Fund) kuwasilisha
upya mchanganuo wa fedha ambazo
zimeonekana kutumika, lakini
mchanganuo wake haukuridhisha.
Fedha hizo ni kiasi cha sh. milioni
43. Na zingine kiasi cha milioni
26.7.
Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali yabaini
uozo Ujenzi
Wakati huo huo, Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) imekerwa na kitendo
cha Wizara ya Ujenzi kutumia sh.
milioni 500 kwa mwaka kwa ajili
ya kulipa kodi za ofisi, wakati
wizara hiyo ina uwezo wa kujenga
ofisi zake.
Mbali na kukerwa na hali hiyo,
kamati imemwagiza Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) kwa
kushirikiana na Wizara hiyo ya
Ujenzi kujenga ofisi ambazo
zitatumika badala ya kutumia fedha
nyingi kulipa kodi.
Hayo yamebainishwa Dar es
Salaam jana na Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Bw.John Cheyo,
wakati wakikagua hesabu za wizara
hiyo.
Bw.Cheyo alisema, haiwezekani
Wizara kubwa kama hiyo na yenye
uwezo kushindwa kujenga majengo
na badala yake kuishia kupanga
huku wakitumia fedha nyingi
ambazo zinaitia hasara Serikali.
Akijibu hoja hiyo Katibu Mkuu
Mtendaji wa Wizara Balozi
Heaberth Mrango, alikiri kuwa
kiasi cha fedha kinacholipwa kwa
mwaka ni kikubwa,lakini akajitetea
kuwa kazi ya kujenga majengo ni ya
wakala wa majengo.
“Mheshimiwa mwenyekiti kazi ya
kujenga ofisi ni ya wakala na mimi
niliishauri Serikali kujenga majengo
yake, lakini imeshindikana kutokana
na ukosefu wa fedha,”alisema
Balozi Mrango.
Katika hatua nyingine kamati
hiyo imeiagiza wizara hiyo kuunda
kamati maalum ndani ya miezi
mitatu ili kuchunguza ujenzi wa
majengo marefu karibu na Ikulu.
Akitoa agizo hilo Bw. Cheyo
alisema kwamba anavyofahamu yeye
Ikulu ni sehemu ya kuheshimika,
lakini TBA wameenda kujenga
majengo marefu jirani na eneo hilo
na akahoji kwamba hawaoni jambo
hilo ni hatari kwa nchi?

3 comments:

  1. Mheshimiwa Mrema na kamati yako. Kazi yenu si ya Kipolisiau ya kuttishia watendaji. kuagiza hakusaidii.tumia mfu wa kistaarabu wa kumshauri mkuu wa kazi wa DED. Yeye kama kiongozi atatumia sheria (Government Regulations)zilizopo amchukulie hatua. Kama ni kumnyima mshahara, kumsimamisha, kumpa likizo au apeleke suala lake wizara ya utumishi ni yeye na sio KAMATI yenu. msifanye kazi za watendaji!

    ReplyDelete
  2. hIVI WEWE ULIE COMMENT HAPO JUU UNAJUA NINI,AU HAO WATU MNAUHUSIANO GANI,??UNAJUA HAWA WATU UNASHINDWA KUWAELEWA.SASA UNASEMA NINI PESA ZILIWE KIJINGA WE SAWA TU.NCHI YETU HII INAWATU AU INA WETU???

    ReplyDelete
  3. NA WEWE UNAE MALAUMU ANONYMOUS WA KWANZA HUJUI ULISEMALO. HAKUNA MTU ANAETETEA PESA ZA UMMA KULIWA 'KIJINGA' BALI HAYA MAMBO YANAENDESHWA KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI.

    MH MREMA NA KAMATI YAKE WANATAKIWA WAFANYE KAZI ZAO KAMA MHIMILI (BUNGE) SIO KUFANYA KAZI ZA MHIMILI MWINGINE (EXECUTIVE) KUANZA KUAMURU WATU WAKATWE MISHAHARA, KUSHUSHA VYEO, KUFUKUZA KAZI, KUHUKUKUMU NK. HAYAO NI MAMBO YA EXECUTIVE NA LEGISLATURE.
    NI KOSA KAMA ALIVYOKOSEA ZITTO KUAGIZA GENERATOR LIONDOLEWE KWA MKUREGENZI WA TANESCO, WABUNGE PAMOJA NA KAZI NZURI WANAYOIFANYA WASICHUPE MIPAKA YA MAMLAKA YAO VINGINEVYO ITAKAKUWA LAWLESS SOCIETY

    ReplyDelete