21 March 2012

Ubinafsishaji viwanda ulete tija kwa watanzania

MAENDELEO ya Taifa
linaloendelea duniani
linahitaji viwanda imara ili
likue kiuchumi ni lazima
liwe na viwanda imara
ambavyo vitatoa msukumo
katika kuchocheo ukuaji wa uchumi na kuinua
soko la ajira.

Tanzania ni moja ya nchi zinazohitaji kuwa na
viwanda ili kuinua uchumi na kupunguza tatizo
la ajira kwa wananchi wake.
Tunaamini kuwa, endapo kutakuwepo
viwanda imara vinavyofanya kazi soko la ajira
litakua kwa kiwango cha juu na kuinua uchumi
wa nchi.
Jumla ya viwanda 74 chini ya wizara ya
viwanda biashara na masoko vilibinafsishwa
kwa lengo likiwa ni kuviongezea nguvu na
kuendelea kuinua uchumi na soko la ajira
nchini.
Pamoja na nia njema ya serikali katika
kubinafsisha viwanda, baadhi ya vimeshindwa
kuendelea na kujikuta vikifa kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo wawekezaji kukosa mitaji
ya kuviendeleza.
Baadhi ya viwanda kufanya vibaya na
kushindwa kufanikisha malengo ya serikali,
vipo vinavyofanya vizuri na kuvuka malengo
ya serikali waliyokubaliana ambapo kati ya
viwanda 74 vilivyobinafsishwa 42 ndivyo
vinafanya vizuri.
Mojawapo ni Kiwanda cha Sukari cha TPC
kilichopo katika wilaya ya Moshi mkoani
Kilimanjaro.
TPC ndicho kiwanda cha sukari kikongwe
nchini ambacho kilichukuliwa na serikali
mwaka 1979 na kubinafsishwa mwaka 2000.
Uzalishaji wake ulikuwa ni tani 36,000 za sukari
kwa mwaka.
Ofisa Mkuu Utawala wa Kampuni ya TPC
Bw. Bw.Jafary Ally anasema, baada ya kiwanda
hicho kubinafsishwa walitakiwa kuongeza
uzalishaji mara mbili kutoka tani 36,000 hadi
kufikia tani 72,000 kwa mwaka.
Bw. Ally anasema, pamoja na kupewa
malengo hayo na serikali kiwanda hicho
kiliweza kufanya kazi na kuongeza jitihada na
kufanikiwa kuvuka lengo hilo kuzalisha tani
85,000 kwa mwaka.
"Kimsingi ni kwamba katika uzalishaji
tumeweza kuvuka lengo la serikali na sasa
tunazalisha tani 350 hadi 500 kwa siku, kwa
mwaka tukizalisha tani 85,000 ambapo ni zidio
la tani 13,000" anasema Bw. Ally.
Anasema, kiwanda hicho kinamiliki eneo
lenye ukubwa wa hekta 16,000, kati ya hizo
8050 zinalimwa miwa kwa ajili ya uzalishaji
wa sukari.
Anaeleza kuwa, kiwanda hicho kinazalisha
miwa tani 800,000 kwa mwaka ambazo
zinazalisha sukari tani 85,000 na kwamba
kiwanda hakijaanza kuchukua miwa kutoka
nje ya kiwanda .
Anasema, katika kiwanda hicho wamekuwa
wakiendesha kilimo cha umwagiliaji kutokana
na upingifu wa mvua ambapo hupokea mvua
milimita 550 pekee.
Anafafanua kuwa, uzalishaji wa miwa katika
kiwanda hicho umekuwa ukikua mwaka hadi
mwaka ambapo hadi kufikia mwaka jana tani
800,000 na kwa mwaka huu wanatarajia kuvuka
uzalishaji huo.
Anasema, wakati kiwanda hicho
kinabinafsishwa usagaji wake ulikuwa chini
lakini kwa sasa wameweza kupandisha na
kufikia tani 160 kwa saa na kwa siku ni tani
3,900.
Anasema, sukari yote inayozalishwa
katika kiwanda hicho inauzwa ndani ya nchi
ambapo tani 70,000 zinauzwa katika mikoa
ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara huku tani
15,000 zikiuzwa katika mikoa ya Tanga na
Singida.
Anasema, pamoja na mafanikio hayo bado
wamejiwekea mikakati mbalimbali ili kuendelea
kuongeza uzalishaji katika kiwanda hicho ikiwa
ni pamoja na kuinua uchumi wa nchi na soko
la ajira.
Anasema, moja ya mikakati waliyojiwekea
ni kuongeza uzalishaji pamoja na kuboresha
Sukari inayozalishwa katika Kiwanda cha TPC ikiwa imehifadhiwa.
miundombinu ya kiwanda ikiwa ni pamoja na
ya umwagiliaji na kuchimba visima .
Anaongeza kuwa, mwaka huu wamejipanga
kuongeza uzalishaji wa miwa kutoka tani
85,000 zilizozalishwa kipindi cha mwaka jana
hadi kufikia tani 90,000.
Anasema, pamoja na mafanikio na mikakati
mbalimbali waliyonayo bado wanakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba
wa maji kwa ajili ya umwagiliaji na uhaba
wa ardhi.
Maji katika kiwanda hiki bado ni tatizo
kubwa kiwandani hapa kwani maji mengi yana
magadi na hata kidogo yaliyopo yamekuwa
yakiibiwa hali ambayo imekuwa ikituletea
shida,anasema.
Afisa Mtendaji Mkuu TPC Bw.Robert
Baissac, anasema, toka kubinafsishwa kwa
kiwanda hicho yapo mafanikio mbalimbali
ambayo wameyapata ikiwa ni pamoja na
kuongeza uzalishaji na kuvuka lengo la
serikali.
Anasema, pamoja na malengo hayo ya
serikali wameweza kuongeza uzalishaji huo
mara dufu kutoka tani 72,000 hadi zilizokuwa
lengo la serikali na kufikia tani 85,000 kwa
mwaka.
Waziri wa Viwanda na Biashara na Masoko
Dkt. Cyril Chami anasema, viwanda vilivyopo
chini ya wizara hiyo 74 vilibinafsishwa na
vilirithiwa kutoka kwa hayati mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Anasema, katika ubinafsishaji wa viwanda
hivyo yapo makubaliano baina ya serikali na
wawekezaji ikiwemo kuongeza kiwango cha
uzalishaji.
An a s ema , k a t i y a v iwa n d a 7 4
vilivyobinafsishwa 42 vimefanya vizuri na
kupita lengo ikiwemo kiwanda hicho, Kiwanda
cha Bia Tanzania (TBL), Kiwanda cha sigara
pamoja na Kiwanda cha Mufindi paper.
Anasema, viwanda 17 kati ya hivyo utendaji
wake sio mzuri bali wa wastani ambapo
vinafanya kazi na kukabiliwa na matatizo
mbalimbali ikiwemo malighafi na masoko.
"Viwanda 15 kati ya 74 vimekufa na havifanyi
kazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
mtaji pamoja na kutokuwepo kwa ujuzi mpya,"
anasema.
Dkt. Chami anasema, shirika Hodhi la
mali za taifa linaendelea na mazungumzo
na wawekezaji wa viwanda vilivyokufa ili
kuangalia uwezekano wa kuvunja mikataba
na kuvikabidhi kwa wawekezaji wenye uwezo
wa kuviendeleza.
Serikali haiwezi kukaa kimya kuviangalia
viwanda vilivyoshindwa kuendelea, inafanya
utaratibu wa kuvirudisha mikononi mwa
serikali kwa kufuata utaratibu na kuwapa
wawekezaji wenye uwezo ili wavifufue na
kufanikisha malengo ya serikali kukuza soko la
ajira hapa nchini, ” anasema Dkt. Chami.
Anasema, nia ya serikali kuvibinafsisha
viwanda ilikuwa kuinua uchumi wa nchi na
soko la ajira lakini kufa kwa viwanda hivyo
kumepelekea malengo na nia njema kushindwa
kufanikiwa. Anasema, serikali inashirikiana na
wawekezaji wa viwanda 17 ambavyo utendaji
kazi wake si wa kuridhisha ili kuangalia
uwezekano wa kuviboresha na kulinda soko la
ajira na huduma nyingine za kijamii.
Pamoja na viwanda 15 kufa pia viko vingine
17 ambavyo vina matatizo ya hapa na pale kama
vile upatikanaji wa malighafi na kubadilika kwa
masoko, lakini vipo viwanda 42 ambavyo kwa
kweli vinafanya kazi nzuri na vimeweza kuvuka
lengo walilokubaliana na serikali anasema Dkt.
Chami.
Anasema, pamoja na viwanda 189 vikubwa
kujengwa pia vimejengwa viwanda 10,237
vidogo katika kipindi hicho cha kuanzia
disemba 2005 hadi kufikia disemba 2011.
Anasema viwanda vipya vitajengwa kulingana
na mahitaji yaliyopo na kwamba vipo viwanda
vingine katika mchakato wa ujenzi kwa lengo
la kuinua uchumi na kupunguza tatizo la ajira
hapa nchini.
"Ni wakati wa viongozi na watanzania
wote kupongeza jitihada mbalimbali ambazo
zimekuwa zikifanywa na serikali na si kubeza
kila kitu, ni vema kama kuna changamoto
zitolewe za kuboresha na si kulalamika na
kulaumu,"anasema Dkt. Chami.

No comments:

Post a Comment