21 March 2012

Tunaunga mkono kauli ya JK

JANA Rais Jakaya Kikwete amepiga marufuku vyama vya ushirika nchini,kuuza majengo yake na pia viajiri watendaji waadilifu wanatakasaidia kuvipatia maendeleo
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika. Alisema majengo hayo yamekuwa yakiuzwa kwa bei ndogo na kutolea mfano lile la mkoani Mwanza ambalo liliuzwa sh. milioni 50 wakati thamani yake ni sh. 500.

Kwanza tunampongeza Rais Kikwete kwa kuliona hilo, kwani kukosekana kwa watumishi wenye uadilifu ndiko kumechagia vyama hivyo kukosa nguvu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Inawezekana tukafufua vyama hivyo, vikawa na nguvu kama ilivyokuwa zamani iwapo vitakuwa na watumishi wenye sifa na uadilifu. Leo hii vyama hivyo havina nguvu kama zamani,kwani baadhi yake vimejaa watendaji wenye roho ya kujinufaisha, badala ya kuviendeleza.

Tunasema tuna ushahidi wa jambo hili upo wazi. Miaka ya nyuma vyama vya ushirika vilikuwa vikimiliki shule za sekondari na vilikuwa na vitega uchumi, lakini leo hii tunazungumza lugha nyingine.

Shule hizo ndipo walisoma watoto wengi wa wakulima ambao leo hii ndiyo tegemeo la taifa. Wakati huo shule za serikali hazikuwa nyingi kama ilivyo sasa, lakini mchango wa vyama vya ushirika na na zile za Jumuiya ya Wazazi zilisaidia sana.

Leo hii shule hizo nyingi hazipo kwani zilibinafsishwa baada ya vyama hivyo kushindwa kuziendesha. Tunawapongeza wale ambao walitambua mchango wa shule hizo na kuamua kuzichukua kwa ajili ya kusaidia kuendeleza vijana wetu.

Tuna imani kuwa kama mwito wa Rais Kikwete utafanyiwa kazi, vyama hivyo vitakuwa na mchango mkubwa katika suala zima la kukuza uchumi. Kinachotakiwa kwa sasa ni watumishi waadilifu wa kutoa vyama hivyo hapa vilipo.

Hatuhitaji viongozi wenye mawazo ya kuuza majengo ya vyama hivyo kwa ajili ya kujinufaisha. Tunahitaji viongozi watakaosukumwa na dhamira ya dhati kuendeleza ushirika.

Hatuhitaji vyama vya ushirika vya kuwakandamiza wakulima, bali vya kuwainua hapo walipo. Haiwezekani leo hii mkulima wa Karagwe alazimishwe kuuza kahawa yake kwa bei ya sh. 400 wakati nchi jirani ya Uganda kilo hiyo hiyo inauzwa kwa sh. 1,000.


1 comment:

  1. Ushirika usilaumiwe kuuza mali zao za kudumu. Wanafuata mtindo wa serikali na mashirika ya umma, Vyama vya wafanyakazi (NUTA nk.) kuuza nyumba, majengo. mashamba, yao, viwanja n.k.

    MTINDO ni huo huo. Kinachomilikiwa na wengi hakina mwenyewe. (THAT WHICH IS OWNED BY MANY BELONGS TO NONE)
    Chakukumbuka ni kuwa kuna wananchi ambao ni wenye mali na baadaye watazidai.

    ReplyDelete