21 March 2012

Kesi ya kumpinga Mnyika Ubungo kuanza kunguruma

Na Rehema Mohamed
MAH A K AMA K u u
Kanda ya Dar es Salaam
leo imeshindwa kuanza
kusikiliza kesi ya kupinga
matokeo ya uchaguzi wa
Jimbo la Ubungo yaliyompa
ushindi Bw.John Mnyika
tiketi ya CHADEMA,
kutokana na mawakili
wa pande zote mbili
kutokabidhiana nyaraka za
maelezo ya awali za kesi
hiyo.

Kesi hiyo ipo mbele ya
Jaji Upendo Msuya, ambapo
jana ilitajwa kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa ambapo
wakili anayemwakilisha
mlalamikaji, Bi.Hawa
Ng’umbi, Bw. Issa Maige
aliieleza mahakama hiyo
kuwa wamegundua kurukwa
utaratibu wa kutokabidhiana
nyaraka hizo.
Alidai kuwa baada ya
pande zote mbili kumaliza
kubadilishana nyaraka hizo,
mahakama ilipaswa kusikiliza
maelezo ya awali pamoja na
mambo yanayobishaniwa
na yasiyo bishaniwa na
hatimaye mahakama hiyo
kuyafanyia kazi mambo
yanayobishaniwa.
Kwa upande wake wakili
wa serikali katika kesi hiyo
Bw.Justus Mulokozi aliieleza
mahakama kuwa ameliona
suala hilo na kwamba
litarahisisha usikilizwaji wa
shauri hilo kwa yale yote
yatakayokubaliwa.
Kutokana na hali hiyo
Jaji Msuya alisema kuwa
mahakama hiyo inakubaliana
na hoja hizo kupitia kanuni
namba 19 ya sheria ya
uchaguzi ya mwaka 2010
kwamba kwanza ilitakiwa
maelezo ya awali yasikilizwe.
Kutokana na hali hiyo
mahakama hiyo imeziamuru
pande zote mbili kufanya
makabidhiano ya nyaraka
za maelezo hayo jana na
kwamba kesi hiyo itaanza
kusikilizwa leo.
Katika kesi hiyo aliyekuwa
mgombea Ubunge wa Jimbo la
Ubungo kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi(CCM), Bi.
Ng’umbi anapinga matokeo
ya uchaguzi mkuu wa jimbo
hilo wa mwaka 2010 ambayo
yalimtangaza Bw. Mnyika
(CHADEMA) mshindi.
Novemba mwaka 2010,
Bi.Ng’umbi alimfungulia
kesi hiyo Na.107/2010
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Bw.Mnyika na
Msimamizi wa Uchaguzi wa
Jimbo la Ubungo, akiiomba
mahakama hiyo itangaze
kuwa matokeo yaliyompa
ushindi mbunge wa sasa ni
batili kwa sababu yalikiuka
taratibu za sheria ya uchaguzi
na kanuni zake ya mwaka
2010 na kwamba mdaiwa
wa kwanza na wa tatu
walishindwa kutimiza wajibu
wao kikamilifu.

No comments:

Post a Comment