21 March 2012

Prof. Mahalu kuendelea kujitetea leo

Na Mwandishi Wetu
KESI ya uhujumu uchumi na
kuisababishia serikali hasara ya zaidi
ya sh.bilioni 2 inayomkabili aliyekuwa
Balozi wa Tanzania Nchini Italia
Prof.Costa Mahalu na mwenzake
inatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.

Kesi hiyo iliyo mbele ya Hakimu
Bw. Ilvin Mugeta, leo itakuja kwa ajili
ya upande wa mashtaka kumhoji Prof.
Mahalu baada ya kufunga utetezi wake.
Katika kesi hiyo.Prof.Mahalu
anatetewa na Wakili Bw. Mabere
Marando, huku pande wa mashtaka
ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali
Bw.Rosiano Lukosi na Bw.Ben
Linkoling.
Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo
ni Bi.Grace Martin, aliyekuwa ofisa
utawala wa ubalozi huo nchini Italia.
Washtakiwa hao kwa pamoja
wanadaiwa walikula njama na kutenda
makosa hayo kwa nyakati na maeneo
tofauti,huko Italia.Katika shtaka la pili,
washtakiwa wanakabiliwa na tuhuma za
kumpotosha mwajiri wao, kupitia hati
ya matumizi.
Ilidai kuwa Septemba 23 mwaka
2002 katika Ubalozi wa Italia jijini
Roma, washtakiwa hao walisaini hati
ya malipo yenye namba D2/9/23/9/02
ikionesha kuwa mauzo ya jengo la
ubalozi ilikuwa ni Euro 3,098,741.58
maelezo ambayo yanadaiwa kuwa ni
ya uongo kwa mwajiri wao.
Katika shtaka la tatu wanadaiwa
kuwa Oktoba Mosi, 2002 washtakiwa
walisaini mkataba wa mauzo ambao
unadaiwa kuwa na maelezo ya uongo

No comments:

Post a Comment