Radhia Ramadhani na Bahati Mohamed
KAMATI ya Michezo ya Mei Mosi mwaka huu, imesema timu 14 kati ya 57 zimethibitisha kushiriki mashindano hayo yanayotarajia kuanza Aprili 16 hadi 29 mwaka huu, ambazo zitafanyika kitaifa jijini Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa kamati hiyo, Award Safari alizitaja baadhi ya timu zilizothibitisha kuwa ni Polisi Tanzania na Wizara ya Maliasili na Utalii.
"Kamati ya Michezo imejipanga vyema katika mashindano hayo ili kuhakikisha mwaka huu yanafana, ikilinganishwa na mwaka jana," alisema.
Safari aliwataka mashabiki wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi, ili kuhamasisha wachezaji wa michezo mbalimbali.
Alisema michezo itakayoshindaniwa kwenye michuano hiyo ni soka, netiboli, riadha mbio ndefu, kuvuta kamba, mbio za baiskeli, karata, bao na drafi.
No comments:
Post a Comment