*Wapiga kura wapinga kauli za Lusinde jukwaani
*Wadai zinakiuka maadili, wamtaja ajirekebishe
*Serikali yarejesha ardhi kwa wananchi ekari 5,000
Na Queen Lema, Arumeru
WANAWAKE wauza nguo katika masoko ya Usa River na Tengeru yaliyopo kwenye Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, wamekishukia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai baadhi ya makada wake hawana maadili wanapokuwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho Bw. Sioi Sumari.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wanawake hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, Mbunge wa Mtera, mkoani Dodoma, Bw. Livingstone Lusinde, amekuwa akitoa lugha za matusi jukwaani bila kujali aina ya watu anaowahutubia.
Walisema Bw. Lusinde ambaye ni kiungo muhimu wa CCM, alitoa lugha ya matusi katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Ngarasero Usa River wakati akimnadi Bw. Sumari.
“Hata kama Bw. Lusinde ana chuki na wapinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anapaswa kutumia lugha nyepesi inayoeleweka.
“Mikutano hii ya kampeni inahudhuliwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo watoto ambao tunawaalibu kimaadili, jambo la msingi vyama vyote vione umuhimu wa kuepuka lugha za matusi ambazo hazisaidii kupata ushindi,” walisema wanawake hao.
Wanawake hao walimtaka Bw. Lusinde kuhakikisha harudii kutumia lugha zisizofaa kwenye kampeni badala yake atumie burasa kumnadi mgombea wao.
Wakati huo huo, siku tatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, Serikali imerejesha zaidi ya ekari 5,000 za ardhi mikononi mwa wakazi wa Kata za Nduruma Mlangarini iliyopo Arumeru Magharibi na Mashono jijini Arusha.
Ardhi hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa zaidi ya miaka 20 na kusababisha wananchi washindwe kulitumia.
Mkuu wa Mkoa huo Bw. Magesa Mulongo, alisema Serikali imeamua kufikia uamuzi wa kurudisha ardhi hiyo kwa wananchi.
“Kwa sasa ardhi hii imerudishwa kwa wananchi hivyo ni mali yao kwa mujibu wa sheria...uamuzi huu umefikiwa na Raisi Jakaya Kikwete baada kusikiliza malalamiko yao ya muda mrefu.
“Viwanda hivi vitaongezwa thamani kwa mujibu wa sera ya matumizi ya ardhi, kila mmiliki atalazimika kupima kiwanja na faida ambayo atapata ni pamoja na kukitumia kama mtaji,” alisema Bw. Mulongo na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha hawauzi ardhi hiyo hadi itakapopimwa.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Goodlucky Ole Medeye, alisema wananchi katika kata hizo wanatakiwa kuweka sera ya ardhi ili kuiboresha.
Katika hatua nyingine, Mwandishi Pamela Mollel, anaripoti kutoka Arumeru kuwa, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, mkoani Rukwa, Bw. Aeshi Hilal (CCM), amesema kampeni za uchaguzi wa Arumeru Mashariki zina usalama mkubwa kuliko ilivyokuwa Igunga, mkoani Tabora.
Bw. Hilal aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza atahakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
“Ujio wangu katika kampeni hizi ni kuhakikisha chama chetu kinatetea jimbo hili, hatumwogopi mtu wala wapinzani, awali nilichukulia Arumeru Mashariki kama sehemu ya vurugu na fujo lakini baada ya kutia mguu, nimegundua kuna utulivu wa kutosha,” alisema Bw. Hilal.
Wakati huo huo, mgombea ubunge wa CCM katika uchaguzi huo Bw. Sioi Sumari, jana alipewa zawadi ya biblia na fimbo iliyotolewa na Kikundi cha Wazee waishio katika mazingira magumu cha 'Sikila Hope For Elderly' kilichopo Sakila wilayani hapa.
Wazee hao walisimamisha msafara wa Bw. Sumari na kumuomba awasaidia kwa sababu wanaishi katikia mazingira magumu.
Hii ni dangaya toto kwani ktk miaka yote walikuwa wapi? hadi hiki kipindi cha uchaguzi ndiyo wajitokeze kurudisha aridhi na kusema wananchi wa kata hiyo wasiuze aridhi hiyo.
ReplyDeleteJe serikali ipo tayari kufidia familia ambazo zimepoteza wapendwa wao na mali zao ktk kata hizo?
Acha upumbavu wewe, tazama hilo gazeti la mwananchi
ReplyDeletelinakotoka huko kenya na chadema wanakokodisha helikoputa, kama wananchi wake wana aridhi
Sasa wewe tukuelewe vipi! Unafaidika na ufisadi? Taratibu, siku zenu zinaanza kuhesabika, maanake hata muwapumbaze vipi wananchi kwa kufanya vioja kama hivi vya kurudisha ardhi wakati wa kuomba kura kwa kudhani kwamba wananchiwataendelea kulala usingizi, hatimaye wataelewa haki zao ni zipi. Huo ndio utakuwa mwisho wa watu kama wewe kuendelea kuwanyanyasa wananchi hawa.
DeleteWANAWAKE OYEE! WASEMENI HAWA CCM WAACHE TU SIO MATUSI PIA WAACHE KUKUCHEZEA MALI ZA WATANZANIA KWA KULINDA MAFISADI WACHACHE WENYE NGUVU ZAIDI YA SERIKALI YA CCM WANAOTESA KINA MAMA, BABA, WATOTO WA TANZANIA.
ReplyDeleteKUWAWEZA MAFISADI HAWA NA WENYE KUTOA MATUSI NI WOTE KUSIMAMA PAMOJA NA KUTOIPIGIA KURA CCM. DAWA YA MAFISADI NI KUIONDOA CCM KWA KURA. IKIONDOA MAFISADI WATANYONGONYEA NA KUTOKOMEA.WATUACHIE AMANI YETU.
WANANCHI HAWANA AMANI KAMA ZAMANI KWA SABABU YA MAFISADI. KILA KUKICHA KILIO NI CHA KIBWA FEDHA NA MALI ZA WATANZANIA HATA RAISI WETU HANA USINGIZI KWA SABABU YA MAFISADI.
KURA INA NGUVU KUBWA. ONA JINSI KURA ILIVYOTISHIA SERIKALI YA CCM IKARUDISHA MASHAMBA YALIYOKUWA YACHUKULIWE NA SERIKALI KUPITIA JWTZ. KURA NI SILAHA KUBWA.
WANANCHI WA NDURUMA CHUKUENI HAKI YENU YA MASHAMBA NA MSIWAPIGIE KURA CCM.
MFANO WA CHUKUA FEDHA CCM NA PIGIA UPINNZANI KURA. CHONDE CHONDE, MKIWARUDISHA MADARAKANI WATATUMIA SERA HIYO HIYO KUWANYANGANYA.
NGUVU YA KURA IMEIBUA JANJA YA CCM ILIYOTAKA KUCHUKUA MASHAMBA HAYO KUPITIA MGONGO WA JWTZ. WALIKUWA WAJE WAYAUZE! SILAHA YA KURA OYEE, OYEE..
HAKUNA HAJA YA MAANDAMANO.
KURA YA SIRI ITAMALIZA MAMBO YOTE.CHA KULINDA KUFA NA KUPONA NI MTU YEYOTE ASIKUNYANGANYE HAKI HII YA KUPIGA KURA AMBAYO NI SILAHA YA KULINDA DEMOKRASIA NA MAENDELEO YA WATU.
MNYANGANYENI MTEI KWANZA SHAMBA MAANA HAKUNA MMERU ALIYE NA SHAMBA HAI AU MOSHI VIJIJINI
ReplyDeleteWEWE HAPO JUU. SOMA GAZETI VIZURI. HAKUNA bEPARI AU MTU ALIYENYANGANYWA ARDHI. MASHAMBA YALIYORUDISHWA KWA WANAKATA NI YALE SERIKALI ILIYOKUWA IMETENGA KWA AJILI YA JESHI NA SIO YENYE TITLE DEED (HATI).
DeleteKATIBA NA KANUNI ZA MATUMIZI YA ARDHI ZINAMLINDA MTEI KAMA ZINAVYOKULINDA WEWE KWENYE ARDHI AU ENEO LAKO LA NYUMBA UNALOPANGA. NCHI YETU INATAWALIWA NA SHERIA NA SIO RAHISI KUMNYANGANYA MTU WMWENYE ARDHI KIHALALI. SERIKALI SIO PUMBAVU, KAMA INGEKUWA HIVYO ILIKWISHA NYAN'GANYA WATU WENGI TU.
HII ARDHI ILIKUWA NI MALI YA WANAKIJIJI IILIYOTAKA KUPORWA NA SERIKALI YA CCM YENYEWE. TISHIO LA KURA NDILO LILILOIRUDISHA ARDHI HIYO KWA WANANCHI.
WAMERU WAMEPIGA KURA NA HATA KAMA CCM INASEMA WATAKOSA MAENDELEO KWA KUITOSA, WANANCHI HAWA WATATUMIA HIYO ARDHI VIZURI JAPOKUWA NI NDOGO.
WAMERU NA WAKAZI WA VIJIJI HIVYO KWA TAARIFA YAKO NI WACHAPA KAZI, WASAFI, WATULIVU NA WASIKIVU WA USHAURI WA KITAALAM.
WATAFUGA NGOMBE NA WATAPATA MAZIWA MENGI TUWANAPELEKA WATOTO WAO SHULE KWA KUTUMIA MAUZO YA MAZIWA, MBOGA, NDIZI, KAHAWA NZURI TU, MITI KULINDA MAZINGIRA N.K. HUSIKII WANA NJAA AU OMBAOMBA
SUBIRI KIPINDI CHA MIAKA MIWILI AU MITATU KAMA HUTAKUTA MAENDELEO YAO YAMEZIDI YALE YALIYOFANYWA CHINI YA UONGOZI WA SERIKALI YA CCM. KAMA NI MAJI WATACHANGIA, BARABARA WANAZICHIMBA, ZAHANATI WATAJENGA N.K.
USIDHANI KAMA BAJETI YA SERIKALI ITAWANYIMA FEDHA. WATAZIPIGANIA NA WATAHAKIKISHA KIDOGO WATAKACHOPATA KIJANA MBUNGE MTARAJIWA NASARI, MADIWANI WAKE NA WATAALAM WATAHAKIKISHA KIMETUMIWA VIZURI.
Hakuna kilicho na mwanzo kikakosa mwisho, Huwezi kumfanya mtu mjinga mda wote. CCM imejisahau na kuendeleza dhana yao kuwa itaendelea kuwafanya Watanzania wajinga maisha yote, imefika wakati wamwsema BASI, kama picha ya Arumeru haiwashtui subirini 2015- YOU CAN FULL SOME PEOPLE SOMETIME, BUT YOU CANT FULL ALL PEOPLE ALL THE TIME.
ReplyDeleteNamshauri Mheshimiwa Livingstone Lusinde (Mb) awaombe radhi Watanzania wote kwa lugha ya matusi aliyoitumia kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki siku za karibuni. Hii ni aibu.
ReplyDeleteMheshimiwa Livingstone ni Kiongozi wa juu katika Taifa letu na anatakiwa kuwa taa/kioo kwa watu wote na hasa watoto wadogo.
MATUSI ALIYOTOA YALIREKODIWA NA KILA MTU ATAKAPOYASIKIA yakirudiwa mara kwa mara WATASIKITIKA KWAMBA TUNA VIONGOZI WASIO NA MAADILI NA HATA WATOTO WAKE WAKIMUULIZA MASWALI KUHUSU ALIYOTAMKA ITABIDI AFUNIKE USO WAKE KWA AIBU KAMA YALIVYOFANYA MANYANI KWENYE KITABU CHA KUSADIKIKA KILICHOANDIKWA NA marehemu Shaban Robert.
Ni vyema wakubwa tuwe watu kuonesha maadili ya juu na wa kuwaangazia wengine na si kuwakwaza.