21 March 2012

Slaa alipua mafisadi

  • Asema wanakimbilia makanisani  kujisafisha
  • Ataka fedha zao zikataliwe zimejaa najisi
  • Asisitiza michango wanayotoa haina uhalali
  •  NEC yatoa karipio kwa CCM, CHADEMA   


Na Queen Lema, Arumeru
VIONGOZI wa makanisa nchini
wametakiwa kuwakimbia wanasiasa
ambao wanafanya ufisadi kwenye
miradi mbalimbali ya wananchi
na kisha kukimbilia makanisani
kujisafisha.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa
Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA)
Dkt. Willibrod Slaa jana wakati
akihutubia mkutano wa kampeni
eneo la Migandini akimnadi
mgombea ubunge wa chama hicho,
Bw. Joshua Nassari.
Dkt. Slaa kwa nyakati tofauti
alisema kila fisadi wa Tanzania
a n a k i m b i l i a m a k a n i s a n i
kujisafisha. Alisema mafisadi hao
wanaokimbilia kwenye madhabahu
wanatia najisi makanisa kwa
kuwa fedha na michango ambayo
wanatoa haina uhalali, bali ni mali
ya Watanzania ambao wanateseka.
“Kila mara unasikia wanaenda
makanisani kutoa misaada ya
mamilioni ya fedha, lakini hizo
fedha si halali... sasa kama si
kutumia jina la Mungu kwa njia
chafu ni nini? Nawasihi ninyi
wachungaji kamwe msikubali
kupokea fedha za mafisadi ambao
wamegundua mbinu mpya ya
kujisafishia makanisani,” alisema
Dkt. Slaa.
Aliongeza kuwa endapo
wachungaji wataendelea kuwapokea
mafisadi hao katika makanisa na
madhehebu yao ni wazi wananchi
wataendelea kupata shida kubwa,
huku nchi nayo ikikosa haki zake
za msingi.
Katika hatua nyingine meneja
kampeni wa mgombea wa chama
hicho, Bw. Izrael Natse, alisema
kuwa kwa sasa wapo baadhi ya
wanasiasa ambao wanatumia neno
la Mungu kufanya maasi.
Bw Izrael aliongeza kuwa
mchungaji ambaye ameitwa kwa
jina la bwana hapaswi kuhongwa
kwa kupewa rushwa ambayo
inalenga kukosesha jamii haki za
msingi, bali mchungaji ambaye
ni imara ni yule ambaye anapinga
ufisadi na wizi ndani ya jamii.
“Leo hapa tuna uchaguzi lakini
wapo wanasisasa ambao wanafanya
kampeni hadi kwenye nyumba
za ibada na kwa maana hiyo
wanawateka wachungaji, sasa
mimi nawaambia kuwa viongozi wa
dini hakikisheni kuwa mnasimamia
haki,”alisema Bw. Izrael.
Naye mgombea ubunge kupitia
chama hicho Bw. Nassari alisema
kuwa ifike mahali ambapo
wachungaji waseme ukweli kwa
kuwa nao wana nafasi kubwa ya
kuweza kusaidia jamii ya Jimbo la
Arumeru Mashariki.
Katika hatua nyingine vyama vya
CCM na CHADEMA vimepewa
onyo kali na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) baada ya kubaini
kukiuka taratibu za kampeni na
uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa
habari Msimamizi wa Uchaguzi,
Bw. Trisias Kagenzi, alisema kuwa
amefikia hatua hiyo mara baada ya
kupokea malalamiko kutoka katika
vyama hivyo hivi karibuni ambavyo
vinashiriki uchaguzi mdogo wa
Jimbo la Arumeru.
Bw Kagenzi aliongeza kuwa
kwa sasa anatoa onyo kali dhidi ya
vyama hivyo viwili, lakini kama
havitasikia ataamua kufuata taratibu
za uchaguzi.
“Hadi sasa uchaguzi umefika
katikati ndani ya jimbo hili, lakini
kuna tofauti za malalamiko kwa
maana hiyo tumetoa onyo kali bila
kujali itikadi ya chama chochote,
na tunachokitaka hapa ni amani
tu ndani ya chama chochote kile”
alisema Bw. Kagenzi.

7 comments:

  1. Nadhani hawa chadema wanamsema mheshiwa Laigwenani mkuu wa wazee wa kimasai pale jirani na arumeru. mi nawaunga mkono.

    ReplyDelete
  2. Ruwaichi amjibu Dr Slaa kama alivyomjiu Wasira. Hv Slaa hajui kuwa Bwana anawataka wote wenye mizigo waende kwake na sio wema tu?

    ReplyDelete
  3. Mafisadi waende Makanisani na Misikitini kuungama kwa WIZI, kutubu na KURUDISHA mali kwa Serikali ya wananchi.

    Makanisa au Misikiti ikipokea michango inayohisiwa ni ya kiufisadi na kuirudisha kwa Serikali ambayo ndiyo iliyoibiwa mali. Viongozi wa Makanisa na Misikiti wasiwe wanafiki.

    Hawa ni watumishi wa Mungu na wamesoma kutambua fedha au mali zilizopatikana isivyo halali.

    Sio lazima wataja ni nani amerudisha mali au fedha. Kibaya ni hayo Makanisa au Misikiti kukumbatia hizo fedha hata kama wanazitumia kwa manufaa ya wananchi. Wampe KAISARI ambaye atazigawa kwa wananchi.

    Wawaonye mafisadi kuacha tabia hiyo kwa kuwa hawa mafisadi wanaweza hata kuangamiza Makanisa na Misikiti kwa tabia zao. Watawatisha na hata watawaua n.k

    ReplyDelete
  4. Mtu kama huna cha kutoa ni vizuri kujikalia kimya. Hata kama ni za ufisadi, huko zinakokwenda zinarudi kimya kimya kwa waliodhulumiwa/ibiwa. Hii fedha mali ya Kaisari bwana. Wewe uliona wapi picha ya Bw. Yesu kwenye hizo noti!!!

    ReplyDelete
  5. kiukweli, makanisa yanatumika kama kivuli cha kuwasafisha mafisadi, kutoa sadaka siyo kosa bali kwenda kanisani mwanasiasa na kujinadi kwamba hanahatia, kwanini asitumie pesa zake kuwatangazia watanzania kupitia majukwaa ya kisiasa kuwa yeye hana hatia? waache dhambi hizo, bigup dr.

    ReplyDelete
  6. Dr. Slaa Wewe ni mpambanaji tunakukubali.
    Ila natofautiana na wewe kidogo kuhusu mafisadi kutoa sadaka. Kimsingi Mwenyezi Mungu anajua afanyalo ndio maana wanazirudisha kwa stail B. Kikubwa hapa ni kwamba, Wachungaji,Mashehe,Mapadri, wahimizeni hao mafisadi kutoa michango mikubwa ili kusaidia wananchi kuchukua fedha zao.
    Baada ya hapo jengeni shule, vituo vya afya na saidieni yatima.

    ReplyDelete
  7. kweli wachungaji mnatupereka siko, lini walitubu hatukumbuki,lini walisema kwamba wanagawa sehemu za mali zao kugawiya masikini,hatujaona na nakumbuka jinsi mlivyokuwa mnapiga kelele hoo kwamba mafisadi wanaharibu nchi.kumbe mlikuwa mnata pesa zao.tunapinga kwa nguvu zote.

    ReplyDelete