22 March 2012

Simba yagundua janja ya Waarabu

Na Zahoro Mlanzi
VINARA wa Ligi Kuu Bara, timu ya Simba, imegundua mbinu zinazotumiwa na wapinzani wao katika Kombe la Shirikisho, ES Setif ya Algeria baada ya kupata DVD za mechi mbalimbali za kimataifa na ligi ya nchini kwao walizocheza.
Timu hizo zitaumana Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya michuano hiyo ambapo Simba ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Kiyovu kwa jumla ya mabao 3-2.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga alisema kikosi chao kipo vizuri na kinaendelea na mazoezi kama kawaida kujianda na mchezo pamoja na ile ya ligi kuu.

"Timu yetu ipo vizuri na inaendelea na mazoezi kama kawaida, baada ya kuwapa mapumziko ya siuku moja baada ya mechi yetu dhidi ya MtibwaSugar, tumeingia kambini katika moja ya hoteli hapa jijini, tumeamua  tusiiweke wazi kwa sasa kutokana na sababu tunazozijua wenyewe," alisema Kamwaga.

Alisema wanajua mchezo huo utakuwa mgumu kwao lakini tayari wamershachukua tahadhari mapema kwani tayari wameshaangalia DVD za mechi zao na kujua ni mbinu zipi wanazotumia, hivyo Kocha Mkuu, Milovan Cirkovic tayari analifanyia kazi hilo kwa kuhakikisha anawaelekeza wachezaji wake.

Alisema pamoja na kuangalia DVD zao, haitakuwa tiba tosha kwao kuibuka na ushindi, wanahitaji nguvu kutoka kwa wanachama wao na maandalizi ya uhakika kuhakikisha hilo linafanikiwa.

Akizungumzia hali zawachezaji kwa ujumla, wote wa katika hali nzuri kiafya isipokuwa Juma Jabu ambaye ataukosa mchezo huo kwa kuendelea na matibabu ya kifundo chake cha mguu wa kushoto.

Aliongeza katika mechi hiyo, viingilio vimepangwa kuwakwa viti vya kijani na bluu ni sh. 5,000, viti vya machungwa ni sh. 10,000, Viti Maalum C (VIP C) ni sh. 15, VIP B ni sh. 20,000 na VIP A ni sh. 30,000.

Alisema tiketi zitaanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam na kuwataka mashabiki, wanachama na wadau wao kujitokeza kwa wingi kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza siku ya mechi.


No comments:

Post a Comment