21 March 2012

Diwani wa CCM ajinyonga

Nickson Mahundi, Ludewa
DIWANI wa Kata ya Mlangali wilayani
Ludewa kwa tiketi ya CCM, Bw.Rudolph
Chaula amekutwa amekufa nyumbani baada
ya kujinyonga kwa kamba.

Msemaji wa madiwani ambaye pia ni
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wa
Wilaya ya Ludewa, Bi.Monika Mchilo,
alisema diwani huyo ambaye alikuwa katibu
wa madiwani aliadimika ghafla kuanzia Machi
19, mwaka huu, ambapo wananchi walianza
kumtafuta bila mafanikio.
Bi. Mchilo aliliambia gazeti hili kuwa baada
ya kumtafuta siku nzima bila mafanikio ndipo
familia yake na wananchi walirudi nyumbani
kwa marehemu na kukuta mwili wa diwani
huyo ukininginia kwenye chumba kimojawapo
cha nyumba yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa
Bw.Evarist Mangala, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo lakini alisema sababu za diwani
huyo kujinyonga bado haijafahamika.
Alisema uchunguzi unaendelea juu ya kifo
hicho. Kamanda Mangala aliwataka wananchi
wa kata hiyo kuwa watulivu wakati uchunguzi
wa jeshi la polisi unaendelea ambapo ameahidi
taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika
kwa uchunguzi.
Bi. Mchilo alitoa salamu za rambirambi kwa
familia ya marehemu na kuwataka kutulia
wakati wakisubiri utaratibu wa Serikali katika
mikpango ya mazishi

No comments:

Post a Comment