*Makamba adai TANESCO inadaiwa mil. 269/-
*Asema hali itakuwa 'tete' zaidi kuanzia Agosti
Na Grace Ndossa
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), linadaiwa sh. bilioni 269 na Kampuni ya Kufua Umeme ya Aggreko ikiwa ndio sababu ya shirika hilo, kushindwa kutoa huduma ya umeme kwa ufanisi.
Kutokana na deni hilo, Kampuni ya Aggreko imelazimika kuzima mitambo yake baada ya kukosa fedha za kununulia mafuta yanayotumika kuendeshea mitambo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Bw. January Makamba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Bw. Makamba alisema, Serikali iliombwa kuikopesha TANESCO sh. bilioni 408, lakini fedha hizo hadi sasa hazijatolewa ili kusaidia kulipa deni hilo.
“Hata kama TANESCO watapewa hizi fedha, kwanza tunapaswa kulipa deni la sh. bilioni 269 na kiasi ambacho kitabaki hakitoshelezi kununua mafuta ya kuendeshea mitambo hii,” alisema.
Alisema Kampuni ya Aggreko ilizima mitambo yake tangu Desemba 2011 kwa sababu ya kukosa fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo.
“Kimsingi tatizo la mgawo wa umeme litarrudi kama zamani kutokana na vyanzo vya maji ambavyo vinatumika kuzalisha umeme kupungua, kwa sasa umeme tunaopata unatokana na vyanzo hivi.
“Maji yaliyopo kwenye mabwawa ni kidogo, ikifika Agosti mwaka huu itakuwa kipindi cha kiangazi sasa hali itakuwa mbaya zaidi, njia pekee ya kuondokana na tatizo hili ni kuharakisha ujenzi wa bomba la gesi ambalo Rais Jakaya Kikwete alitoa tamko lijengwe kwa miezi 18 tangu 2011,” alisema Bw. Makamba.
Alisema kukamilika kwa bomba hilo, kutaondoa mgawo kwani umeme wa uhakika utakuwa ukipatikana muda wote.
“Kama tutaendelea kuzalisha umeme kwa kutegemea mafuta, nchi yetu itaelekea kubaya kwani gharama za mafuta zinaongezeka siku hadi siku,” alisema.
Kuhusu utaratibu mpya wa kuagiza mafuta kwa pamoja ambao umeanzishwa hivi karibuni kwa Sheria ya Bunge, Bw. Makamba alisema haujasaidia kupunguza bei ya nishati kama ilivyotarajiwa.
Akizungumza na wadau wa mafuta, Bw. Makamba alisema hivi sasa kamati yake itakaa na kupitia upya kanuni na sheria ili kuangalia njia mbadala za kupunguza bei ya nishati hiyo kama ilivyokusudiwa.
Alisema kati ya kampuni zilizokubaliwa kununua mafuta kwa pamoja, hadi sasa zabuni mbili zimeagizwa na mara ya kwanza ilikuwa Januari na Februari.
Aliongeza kuwa, kipindi hicho ziliingia meli 16 zenye shehena ya mafuta ambapo awamu ya pili ilikuwa iwe Machi na Aprili mwaka huu kwa kuingia meli 17 lakini hadi sasa zimeingia meli mbili tu.
Bw. Makamba alisema meli zimekuwa zikichelewa tofauti na walivyokubaliana kuwa zitaingia zote ambapo changamoto iliyopo ni bei ambayo haijashuka.
Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi wa Masoko kutoka Shirika la Maedeleo ya Petroli nchini (TPDC), Bw. Leo Lyayuke, alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto nne.
Changamoto hizo ni kampuni za kuagiza mafuta, upatikanaji wa zabuni, ongezeko la bei na uchelewaji wa meli.
Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Godwin Samuel, alisema imebainika baadhi ya mafuta yanayoingizwa nchini hasa petroli hayana ubora wa kutosha.
Alisema kutokana na hali hiyo, hivi sasa wanachukua sampuli ya mafuta yanayobaki bandarini na kuyapeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini yana matatizo gani
Mimi niliunga mkono Mhe.Zito kuondoa jenereta kwa mkurugenzi wa umeme ili mkurugenzi aone jinsi raia tunavyopata adha ya umeme.Hawa wakubwa wao majumbani kwao umeme haukatiki maisha yao yote watajuaje kama raia tuna shida??hata wangekata hata umeme ikulu,kwa mawaziri na viongozi mbalimbali,ili kama ni mgao basi kila raia ahusike,siyo kuonea walala hoi tu.Mkurugenzi anasema eti ipo kwenye mkataba si waliompa huo mkataba ni wale wale wenzao sasa anajitetea nini.Hatakama ipo katika mkataba nani aliandika huo mkataba.Hauwezi kubadirishwa,mbona tunabadirisha katiba ya nchi.Itakuwaje ajira ya mtu mmoja.Acheni ujinga,onja joto ya jiwe.Sisi raia tunalia mnadhani hatutaki raha.Raha iliwekwa kwa ajili yenu tu??Acheni ujinga.Na hii nawambia viongozi wanahusika katika nyanja zote kuna mikokno ya mafisadi humo.Kinashindikana nini kila kitu tunacho hapa Tanzania,wasomi tunao,gesi ipo,pesa za madini zipo,lakini mnatoa misamaha ya kodi kwa nini,na baadae mnaomba misaada,nashangaa hata hizo nchi zinaZOTOA MISAADA.wATUNYIME ILI AKILI IKAE SAWA.kILA WAKATI ET TUMEPEWA BIL KADHAA NA NCHI AU SHIRIKA FULANI,WAKATI MNASAMEHE MAKODI AU HAO WANATOA MISAADA NDO WANACHUKUA MADINI,NA URENIUM??MTAMBIE.NCHI UTAFIKIRI HAKUNA WASOMI.MSOMELE MCHIBHO,KAMA MALINGO ANAVYOIMBA??TAFAKARI.
ReplyDelete