*Amchoma kisu kifuani, akimbilia polisi
Na Masau Bwire
MKAZI wa Temeke Mikoroshini Dar es Salaam, Bw. Fikiri Aloyce (31), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumuua mkewe Bi. Kanizia Magnus (26), baada ya kumchoma kisu kifuani.
Taarifa zilitotufikia kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe ambako mtuhumiwa anashikiliwa, zimesema Bw. Aloyce maarufu kwa jina la 'Pondamali' ambaye ni fundi bomba, alitenda kosa hilo usiku wa Ijumaa iliyopita nyumbani kwa wakwe zake Kiembe Samaki.
Wakizungumza na Majira kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, ndugu wa marehemu walisema Bw. Aloyce alikuwa na mazoea ya kumpiga mkewe mara kwa mara.
“Mkewe alikuwa akimshauri mumewe awe mwaminifu katika ndoa yao lakini hakusikia hivyo marehemu alikuwa akikusanya virago vyake mara kwa mara na kurudi nyumbani kwao.
“Siku 30 zilizopita, wanandoa hawa hawakuwa na mawasiliano hadi siku ya tukio ambapo Bw. Aloyce, alifika nyumbani kwa wakwe saa tano asubuhi na kulakiwa vizuri wakiamini anakwenda kusuruhisha tofauti iliyojitokeza na mkewe kumbe alikuwa na lake moyoni,” alisema ndugu wa karibu na Bi. Magnus.
Alisema wanandoa hao walikula chakula cha mchana na usiku pamoja huku wakizungumza na kucheka pamoja kumbe furaha hiyo ilikuwa ya kuagana na mkewe.
“Baba mzazi wa Bi. Magnus alimshauri mwanaye asahau yaliyopita na kurejea kwa mumewe wakalee familia lakini mtoto alipingana na baba yake na kusema hawezi kurudi kutokana na manyanyaso anayopata ambayo siku moja yatakuja kumsababishia kifo,” alisema mwanafamilia aliyezungumza na Majira.
Alisema ilipofika saa nne usiku, Bw. Aloyce aliaga ili aondoke ambapo mkewe na mwanae, walimsindikiza lakini wakiwa umbali wa meta 50 kutoka nyumbani kwa wakwe zake, Bw. Aloyce alichomoa kisu kiunoni na kumpiga mkewe kifuani.
Bi. Magnus alianguka chini na kupoteza maisha papo hapo mbele ya mwanawe aliyekimbia hadi nyumbani na kuwasimlia babu na bibi yaliyomsibu mama yake.
“Wazazi wa Bi. Magnus waliongozana na mjukuu wao hadi eneo la tukio na kumkuta mtoto wao akiwa ameaga dunia na kisu kikiwa kifuani huku damu nyingi zikiendelea kumtoka.
“Waliangua kilio na kupiga kelele kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kuanza kumfukuza muuaji bila mafanikio,” alisema.
Alisema Bw. Aloyce alikwenda kujisalimisha Kituo Kidogo cha Polisi Vingunguti na kudai amemjeruhi mkewe kwa kisu ambapo polisi baada ya kupaata taarifa za kifo cha Bi. Magnus, mtuhumiwa alihamishiwa Kituo cha Polisi Chang'ombe kwa mahojiano zaidi.
Watu kama hao wanatakiwa kupata adhabu kali na kama kunauwezekano nao wauliwe itafanya watu wenye tabia kama za Aloyce waache. Maana ni kipigo kikubwa kwa familia waliompoteza binti yao na kwa mtoto hatasahau maisha yake yote
ReplyDeleteAMA KWELI WANAUME TUNAELEKEA KUANGAMIA, KWA NINI HIVI? KAMA MTU ANATAKA KUFA SI AFE MWENYEWE BADALA YA KUUA MWANADAUMU MWENZIE?
DeleteMUNGU AILAZA PEMA ROHO YA MAREHEMU BI. MAGNUS.
Huyu jamaa anastahili kunyongwa, kwa kitendo cha kinyama alichokifanya ni cha hatari sana kwa jamii, kesi kama hizi sidhani kwamba zinahitaji muda mrefu wa mahujiano apewe haki inayostahili,
DeleteNchi yetu haieleweki,hata kama kaua wakihonga hela ataenda jela mwaka mmoja unamwona mtaani.Kuna watu majambazi yanaua na polisi wanajua na picha zao zipo vituoni,lakini wakikamatwa muda si mwingi unawaona mtaani tena,nchi hii inashida kubwa na kinachosababisha ni rushwa polisi hawaaminiki karibia asilimia 70 hivi.Ukimpa siri polisi na huyo mtu atakamatwa lakini akitoa pesa ya kuwatosha utajikuta siri imefichuliwa.Sasa ushirikiano wa polisi na raia uko wapi eti ulinzi silikishi.Maneno mengi hakuna vitendo.Nikiwa rais nang'oa wote watu au idara zilizo na halufu ya rushwa.Kwa sababu hata viongozi wanahusika katika mambo fulani ndo maana jambo likitokea linapigwa danadana.Wewe uibiwe vitu na majambazi ukienda kuripoti utawaona kweli wanafika kwako,lakini sura na maneno yao ni ya ili utoe kitu kidogo jambo lishughurikiwe bila hivyo hakuna kinachoendelea wakati ni kazi yao.Kiongozi akiibiwa hata rais atatoa tamko hao watu wapatikane na kweli siku mbili nyingi watu hao waliofanya.Je haki iko wapi?????? Haya mambo yakitokea kwa raia polisi wangefanya haraka na kukamata watuhumiwa haraka hivyo.Jesi letu la polisi na serikali yake,watu wasingeiponda mawe kwa maneno.Hiyo ndo hali halisi ya Tanzagiza.Sasa kuna haja gani kuwa na polisi eti wanalinda raia na mali zao.Si hivyo wanalinda wakubwa na mali zao.Kalakabaho.Chadema juu.
ReplyDeletejamani inatisha watu wamwogope mungu
Deletesomeni maandiko siku za mwisho wanadamu watakuwa na roho za shetani
ReplyDelete