21 March 2012

CHADEMA yapigwa kombora Arumeru

CCM  yadai wafadhili wao wameisusa
Pamela Mollel, Arumeru

C H A M A C h a M a p i n d u z i
(CCM) kimesema siri ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kutembeza bakuli ya
michango inatokana na wafadhili
wake kukinyima fedha baada
ya Serikali kukataa shinikizo
lililotolewa na Waziri Mkuu wa
Uingereza David Cameroon, la
kutaka nchi zote rafiki na vyama
vyote vya kisiasa kukubali ndoa ya
jinsia moja.
Hayo yalisemwa na mjini hapa
jana na Mkuu wa Kampeni wa
CCM Bw. Mwigulu Nchemba, kwa
nyakati tofauti wakati akihutubia
mikutano ya kampeni ya kumnadi
mgombea wa chama hicho, Bw.
Sioi Sumari.
Bw. Nchemba aliipongeza
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
kwa msimamo wa kukataa shinikizo
la Uingereza la kutaka ndoa za jinsia
moja zisikubalike nchini.
“CCM na Watanzania wote
wanaunga mkono msimamo huo
na hivyo tuko tayari kukosa misaada
kuliko kukubali ndoa za jinsia
moja,” alisema.
Aliwaambia wananchi kwamba
siri ya CHADEMA kutembeza
bakuli katika mikutano ya hadhara
kwa wanachama wake ili wachangie
kampeni ni kutokana na wafadhili
wa chama chao Consevative cha
Uingereza kinachoongozwa na
Waziri Mkuu David Cameroon
kukinyima fedha za misaada
kutokana na Serikali ya Rais
Kikwete kukataa kuunga mkono
suala hilo.
Alisema kuwa tangu chama
hicho kianzishwe hakijawahi hata
siku moja kutembeza bakuli na
kuwakamua wanachama na wapenzi
wake kwenye mikutano ya hadhara
baada ya Serikali kukataa masharti
ya ushoga na ndoa za jinsia moja
kama ilivyokuwa imependekezwa
na Uingereza sasa kimeibua mbinu
hiyo ya kuwakamua wanachama na
wafuasi wake.
Aliongeza kuwa katika uchaguzi
mdogo uliofanyika jimbo la Igunga,
mkoani Tabora mwaka jana, chama
hicho kilikuwa na fedha nyingi
ambazo kilipewa msaada na ndio
maana kiliweza kusumbua, lakini
safari hii wamenyimwa ndio maana
hata viongozi wao wa kitaifa
ushiriki wao kwenye kampeni
hizo za Arumeru Mashariki ni wa
kusuasua.
“Haiwezekani ghafla fedha
w a l i z o k u w a w a k i z i f a n y i a
mbwembwe kwenye uchaguzi
wa Igunga zikawa hazipo na
hapa wameshindwa kuonesha
m b w e m b w e h i z o k u m b e
wamenyimwa fedha kutoka kwa
wafadhili sasa kazi waliyobakiza
ni kuwakamua wanachama na
wafuasi wao kwa kutembeza bakuli
kwenye mikutano kama alivyofanya
Mwenyekiti wa Taifa (Bw. Freeman
Mbowe),” alisema Bw. Mwigulu.
Aliwaambia wananchi kuwa
wapinzani wameshindwa kueleza
sera na matokeo yake wanaeneza
propaganda za uongo, lugha za
matusi na chuki.
“Sisi tunaeleza ilani na sera za
kumsaidia mwananchi kuboresha
maisha sanjari na kutatua kero
zilizopo hivyo mchagueni mgombea
wa CCM ambaye sera za chama
chake ndizo zinazotekelezwa na
serikali iliyopo madarakani,”alisema

5 comments:

  1. Amakweli CCM NI vilaza kweli hata juzi wanaomba mbumge achaguliwe ili afutwe machozi leo anajifanya wamekataa ushoga, bado hawaja banwa mbavu watakubali tu wasitudanganye.
    CCM wameuza nyumba za watumishi hii ni zambi kubwa haitasahaulika kamwe. Leo mnajifanya mnazijua changamoto za Arumeru muda wote muwepo madarakani mumeshindwa leo kuna nini kipya mtafanya huu ni WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  2. Amakweli CCM NI vilaza kweli hata juzi wanaomba mbumge achaguliwe ili afutwe machozi leo anajifanya wamekataa ushoga, bado hawaja banwa mbavu watakubali tu wasitudanganye.
    CCM wameuza nyumba za watumishi hii ni zambi kubwa haitasahaulika kamwe. Leo mnajifanya mnazijua changamoto za Arumeru muda wote muwepo madarakani mumeshindwa leo kuna nini kipya mtafanya huu ni WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  3. Nchemba sasa dhahiri unashindwa kunadi sera za ccm watu wa meru hatuitaji kusikia habari za wafadhili wa chadema,wanachama wao na mashabiki wao wanavyochangishana pesa kwenye mikutano yao.kama hawana pesa za kampeni hatutaki kujua,tunasikia sera zao,tunasikia watatufanyia nini watu wa meru.watanzania wa sasa si wa kuwambiwa propaganda hata wa vijijini ambao tumekuwa tukiwaona hawaeliwi kiti, hivi sasa ni waelewa kuliko wa mji.chadema mtumie vizuri huu udhaifu wa nchemba,wasira,lusinde,sendeka ambao wameonyesha kushindwa kumnadi mgombea wao. .

    ReplyDelete
  4. CCM si ndiyo mliohusika kwa njia moja au nyingine kiba fadha za Benki Kuu (BOT)?

    Fedha za Meremeta, za RADA, Za BoT jengo pacha n.k. mlizopitisha kwa wanaowapa mafuta bure ya kuendeshea magari zikiisha mtaenda wapi? Mlizokuwa mnachota kwenye mashirika ya Umma zikiisha mtaenda wapi?

    Tutawanyima Ruzuku kwa kutowapigia kura tuone na nyie mtatembeza bakuli wapi. ARUMERU wanyimeni kura.

    CHADEMA ni ya wananchi na wingi wa UMMA wa watu utawapa fedha. Hata kama ni shilingi 100 kila mmoja zitatosha. Chadema haijazoea kutanua na frdha kama ccm.

    ReplyDelete
  5. MTU ANAITWA NCHEMBE HIV AMESOMA WAPI? MBONA UELEWA WAKE NI MDOGO KWA KILA JAMBO? ANATUAMBIA NIN WATANZANIA? BILA SHAKA NAE ANALINDA MASIRAHI YAKE CCM LAKIN AJIFUNZE KUJENGA HOJA

    ReplyDelete