Na Agnes Mwaijega
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekiri baadhi ya wanachama wake kukosa maadili lakini sababu hiyo haiwezi kusababisha chama hicho kife kama inavyosemwa na baadhi ya watu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari siku moja baada ya baada ya makada wa chama hicho kukitabirria kifo walipoojiwa katika kipindi cha Je, tutafika kinachorushwa na Kituo cha Channe Ten.
Makada hao ni Bw. Ibrahim Kaduma, Dkt. Hassy Kitine na Bw. Joseph Butiku ambapo katika kipindi hicho, makada hao walidai CCM ya sasa si kama ile ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwani kimekuwa cha kibiashara na maslai binafsi jambo ambalo linaashiria hakiwezi kudumu.
Bw. Nnauye alisema CCM bado ni taasisi imara yenye vijana wenye nguvu na uwezo wa kukifanya kiendelee kuwepo milele.
“Naomba niwahakikishie Watanzania na wanachama wote wa CCM kuwa chama chetu hakitakufa hata siku moja kama wanavyoitabiria,
sisi tunatambua kuwa kuna tatizo la maadili ndani ya chama ndiyo maana Kikao cha Halmashauri Kuu kilichokaa Aprili 2011, kilipendekeza suala la kujivua gamba.
“Tumawashukuru kwa mawazo yao, binafsi nayaheshimu na tumeyasikia tutaendelea kuyatekeleza lakini wajue kuwa tayari yalishaanza kufanyiwa kazi muda mrefu,” alisema.
Aliongeza kuwa, CCM ina uwezo mkubwa wa kujitathmini kiutendaji na kutatua matatizo ya kichama lakini hakiwezi kufa bali kitaendelea kuwepo na kutekeleza makukumu yake kwa kuzingatia kanuni na sheria.
CCM ITAKUFA IKIWA ITAENDELEA KUWADHARAU WANACHAMA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA KWA KUWALINDA WEZI (MAFISADI) WALIOKUPUA FEDHA ZA WANANCHI.
ReplyDeleteUSEMI WA KUWA WAKO WACHACHE SI SAWA. HATA FISADI MMOJA ANAWEZA KUKOMBA FEDHA NYINGI TU NA SIO VISENTI.
WEWE NAPE UNATISHWA NA MAFISADI NDIO MAANA UNARUDI NYUMA KATIKA MAPAMBANO.
TETEA WANACHAMA NA WANANCHI KAMA ANAVYOFANYA KIJANA SHUPAVU MALEMA WA ANC AFRIKA KUSINI.
ANAWAANDAMA VIONGOZI WA ANC WALIOKOMBA FEDHA ZAO WAKAWASAHAU WANACHAMA NA WANANCHI WAO.
CCM ISIJILINGANISHE NA ANC HATA SIKU MOJA. ANC ILICHUKUA MALI NA FEDHA ZILIZOKUWA MIKONONI MWA SERIKALI YA MAKABURU. CCM ILICHUKUWA MALI NA FEDHA ZA SERIKALI YA WANANCHI WA TANZANIA. MWALIMU WETU NYERERE AKIONGOZA SERIKALI YA CHAMA CHA TANU ALICHUKUA MALI ZILIZOKUWA MIKONONI MWA SERIKALI YA WAKOLONI NA KUZIWEKA MIKONONI MWA SERIKALI YA WANANCCHI WA TANZANIA KUPITIA MASHIRIKA YA UMMA.
NI MALI HIZI ZA WANANCHI AMBAZO CCM ILICHUKUA NA KUENDELEA KUCHUKUA. TUKUMBUKE FEDHA WALICHANGA KUPITIA KODI WANANCHI WOTE(HATA MTOTO MDOGO) KWA KUNUNUA BIDHAA KAMA BIA , KANGA, NA MALI NYINGINEKUTOKA VIWANDA VILIVYOKUWA VYA UMMA, KUMBUKA FEDHA ZILIZOCHOTWA KUTOKA MASHIRIKA YA UMMA KAMA SIGARA, MABENKI, BIMA, MIFUKO YA JAMII N.K.
CCM IACHE KUIHUSISHA ANC NA MATUMIZI YA FEDHA HIZI ZA WANANCHI KATIKA MABIASHARA AMBAYO CCM INAYOTAKA KUANZISHA. WANANCHI WAKO MACHO WALISTUKIA CCM KWENYE MPANGO WA EPA, MREMETA N.K. CHONDECHONDE WANANCHI WASIAMUE KUJA KUZIDAI MALI HIZI KISHERIA MBELENI. WCHANGISHENI WANACHAMA WENU MIL.6 NA SIO MAKAMPUNI BINAFSI. CCM ILIKWISHA FILISI NA KUZIKA SUKITA, BIASHARA YA SASA MTAIWEZA AMBAPO KUNA USHINDANI?
USHAURI: - VIJANA WA CCM MWALIKENI KIJANA SHUPAVU MALEMA WA ANC KWENYE SEMINA ZENU AWAELEZE JINSI UONGOZI WA ANC YA SASA UNAVYOWATESA WANANCHI WA SOUTH. AJIRA, UMASKINI, KUTOKANA NA WAZUNGU NA WEUSI WACHACHE KUPITIA CHAMA CHAO NDIO WENYE KUJILIMBIKIZIA MALI SASA. JIULIZENI KUWA KUNA WAFANYAKAZI AU WAWEKEZAJI WEUSI WA SOUTH WALIOKO TANZANIA?
UVCCM BADILISHENI HALI HII KUOKOA CCM ISIFE.
MANENO MENGI NA WOGA BILA MATENDO HAYATASAIDIA.
MSIWE MASHABIKI AU VUVUZELA ZA VIONGOZI WENU WA CCM. SEMINI UKWELI NA WANACHAMA NA WANANCHI WATAWAPENDA.
Wewe Bwana mdogo Nape unajipa moyo sawa haitakufa lakini utabaki uanachama jina lakini kura zetu hupati kutoka humu kwenye chama,hupati kabisa mi nakwambia.Mnaongea tu hakuna matendo.Maneno mengi sana siasa siasa tu hakuna chochote,wezi walioiba pesa wako wapi,wakina Maumba mnawafunga miaka 2 na ameshatoka,huku kakomba pesa kibao,kama siyosiasa nini.Wakina Papii kocha Nguza Viking wanaozea jela,kwa mambo ya kijinga.Waondoeni waje uraiani.Acheni hizo.Magamba yako wapi siasa tu.Mtaona mwaka 2015 si mbali.
ReplyDelete