*Yatuhutumiwa kumwaga pesa, Sioi azidi kuchafuliwa
Na Waandishi Wetu, Arumeru
CHAMA cha Wakulima (AFP), kimesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinafanya biashara haramu ya kununua shahada za kura na matumizi makubwa ya fedha kinyume na utaratibu katika kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Rashid Rai, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema kumekuwa na matumizi makubwa ya fedha kwenye kampeni zinazoendelea jimboni hapa lakini vyombo vya dola vimekaa kimya bila kuchukua hatua.
“Tunalaani matusi ya nguoni katika mikutano ya kampeni kwani kufanya hivi ni kinyume na taratibu za uchaguzi lakini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bw. John Tendwa, ameendelea kufumbia macho suala hili.
“Hadi sasa, kuna kila dalili kuwa CCM inatumia fedha nyingi kununua shahada za wapiga kura na kutumia matusi katika kampeni zao, sisi tunasema dawa ya kukomesha biashara hii ni kuleta fomu namba 17,” alisema Bw. Rai.
Aliongeza kuwa, hadi sasa CCM haijaleta maendeleo yoyote katika jimbo hilo ndiyo maana wanatumia majukwaa kutukana matusi ambayo hayafai.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, ameitaka CCM kuacha tabia ya kuwatumia mabalozi wa nyumba 10 kipindi cha uchaguzi na kuwaacha katika hali ya umaskini.
Bw. Mbowe aliyasema hayo jana katika Viwanja vya Maksoro, vilivyopo Kata ya Akeri, wakati akimnadi mgombea mbunge kwa tiketi ya chama hicho Bw. Joshua Nassari.
“Mara nyingi CCM inawatumia mabalozi wa nyumba 10 kipindi cha uchaguzi lakini ukiisha, wanawatupa kama uchafu, chama hiki hakina huruma hata kwa watu wake wanaowatumia,” alisema.
Alisema CHADEMA ina uhakika wa kushinda uchaguzi huo kwa asilimia 95 kwa sababu ya kufanya kampeni za kistaarabu.
Katika hatua nyingine, Meneja Kampeni wa chama hicho Bw. Vincent Nyerere aliwataka wakazi wa jimbo hilo kuwasemehe viongozi wa CCM kwani hawajui wafanyalo.
Katika hali isiyo ya kawaida, watu wasiofahamika wanadaiwa kusambaza waraka kwa wapiga kura ili wasimpigie kura mgombea wa CCM, Bw. Sioi Sumari kwa madai kuwa, kama watamchagua watatengeneza utawala wa kifalme.
Waraka huo unajieleza kuwa wasambazaji ni Kamati Maalumu ya kupambana na ufisadi hivyo kumchagua Bw. Sumari ni sawa na kukuza mtandao huo.
Sehemu ya waraka huo inasomeka kuwa “Wameshachoka na tabia ya mafisadi kujitokeza katika mambo mbalimbali yanahusu demokrasia nchini,”.
Wakati huo huo, Mwandishi Pamela Mollel anaripoti kuwa, Mbunge wa Arumeru Magharibi Bw. Goodluck Ole Medeye (CCM),
amewataka wakazi wa Arumeru Mashariki kuwa makini na kauli za Katibu Mkuu wa (CHADEMA), Dkt. Wilbrod Slaa kuwa chama hicho kitawatulia matatizo ya ardhi endapo watamchagua mgombea wao Bw. Nassari.
Alisema Dkt. Slaa ni muongo kwani aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Karatu kwa zaidi ya miaka 15 lakin alishinwa kutatua tatizo la ardhi ambapo hadi sasa kuna zaidi ya mashamb 32 ambayo yanamilikiwa na wawekezaji wakubwa.
Bw. Medee aliyasema hayo jana wakati akimnadi Bw. Sumari katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Sing'isi Seela.
“Mchagueni Bw, Sumari ili niwe namkumbusha kuhusu utekelezaji wa kero za migogoro ndani ya jimbo hili, Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti kutatua kero ya ardhi na hivi sasa itatwaa mashamba yote yanayomilikiwa na watu binafsi kama hayajaendelezwa ili wapewe wananchi,” alisema.
Alisema mashamba hayo ni pamoja na Valeska, Madira na shamba la Tanzania Plantation na tayari ameanza ziara ya kuyatembelea.
Wacha kuwa Danganya wanaArumeru Mashariki kwa sababu Tangu tumepata Uhuru jimbo hilo lilikuwa linaongozwa na Chama Tawala.Hakufanya Maendeleo yoyote yale.Leo unathubutu kutoa Ahadi Nzito kama hiyo huoni Aibu kusema wakati huu wa Mwezi wa Kwaresma?
ReplyDeleteHUYU MWAKILISHI WA NEC (MSIMAMIZI WA UCHAGUZI HASIKII MALAMIKO YA YANAYOTOLEWA NA CHADEMA NA CCM? AU HIZI TAARIFA ZA MAGAZETI NI POROJO?
ReplyDeleteVIONGOZI WA NEC WANAVYOTUAMBIA WANAONYA CCM NA CHADEMA KWA PAMOJA. INA MAANA KATI YAO HAWEZI KUPATIKANA MCHOKOZI AU MWOVU? NEC ATAJE MKOSAJI NA UAMUZIAU ADHABU KISHERIA NDIO AWAONYE. ASIOGOPE, KAMA CCM WANASEMA WATAKIMBILIA MSITUNI SIO KOSA? CCM WAKILLALAMIKA WANACHAMA WAO WAMEPIGWA MAWE NA WA CHADEMA SIO KOSA? NAO WANACHAMA WA CHADEMA WAKIPIGWA HADI KUUMIZWA SEHEMU ZA SIRI, WAKITUKANWA MATUSI YA NGUONI NA BAADHI WA VIONGOZI NA MASHABIKI WA CCM, KWA NINI NEC ISITAMKE KUWA CHAMA KIMOJAWAPO KIMEKOSA? AU NEC INANGOJA HADI UCHAGUZI UFANYIKE ILI SERIKALI IJE KUTUMIA FEDHA NYINGI NA MUDA KUSHUGHULIKIA KESI ZA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI? KAMA BABA NEC IAMUE NANI MKOSAJI HATA KAMA KESI ITAPELEKWA POLISI.
HAPA KUNA WASIWASI KIONGOZI WA NEC ANA UPENDELEO FULANI KWA MASLAHI YA CHAMA
KIMOJAWAPO AU ANA NIA YA WATU KUUMIZANA.
NEC OKOA MATATIZO SISI WANANCHI TUNA UWEZO WA KUSOMA KATI YA MISTARI KUEELEWA UNA NIA GANI. TENDA HAKI.
Nani alikwambia kuna NEC,hiyo ni NEC ya ccm,ndo maana wananyamaza wakiulizwa wanasema hawajapata habari.Siri ni moja tu kuwanyima kura hawa ccm.Kwani hao NEC HAWAONI AU KUSIKIA MTU ALIYE NA AKILI TIMAMU ANAJUA KINACHOENDELEA KUWA NEC IKO UPANDE WA CCM.HILI N I JAMBO LA WAZI WAzi si la kuuliza mtu.Kwa nini uhangaike hata hao polisi hakuna kitu.
ReplyDeleteHIVI NDG WANANCHI WA TANZANIA NA ARUMERU CCM IMETAWALA TOKA UHURU MIAKA 5O ZAIDI,LEO UTANGAZE ETI UTAMLETEA MTANZANIA MAENDELEO,AU MWANA ARUMERU HIVI NI AKILI AU KAMASI.ACHANA KABISA NA CCM.
waandishi wenyewe ni rushwa tu,wanapewa mahela hao kuandika habari za chama fulani.
ReplyDelete