30 March 2012

Arumeru Mashariki hapatoshi

  • Lala salama yatawaliwa na vituko vingi 
  • Kigogo CCM adaiwa kudakwa na rushwa
  • Mbowe arushiwa kombora na lusinde
Chama cha mapinduzi (CCM) kimedai viongozi wa chadema wamekuwa wakiwapa wafuasi wake pombe kali aina ya viroba kwa lenga la kuharibu mikutano yao.inayofanyika katika maeneo
mbalimbali.
Pamoja na hilo, pia kimemtupia
kombora mwenyekiti wa Chadema,
Bw. Freeman Mbowe, kwa kujifanya
mpambanaji wakati anaishi kwa
kutegemea mali za urithi za wazazi
na babu zake.
Madai hayo yalitolewa na Mbunge
wa Jimbo la Mtera, Bw. Livingstone
Lusinde, wakati akihutubia mkutano
ya kampeni katika kijiji cha Njeku
wilayani Arumeru jana wakati
akimnadi mgombea wa CCM
Bw.Sioi Sumari .
Alisisitiza kuwa Chadema
inawanunulia vijana viroba vya
pombe kwa lengo la kufanya fujo na
vurugu kwenye mikutano ya chama
hicho, kitendo ambacho ni kinyume
na sheria za uchaguzi.
Alidai kuwa wafuasi hao
wakiongozwa na mbunge wa Jimbo
la Arusha Mjini, Bw. Godbless
Lema wamekuwa wakipita kwenye
mikutano ya kampeni ya CCM
na kuzomea mikutano yao huku
wakifanya fujo, jambo ambalo si
la kistaarabu hata kidogo.
"Nawashangaa Chadema kwa
kuwapa wafuasi wao pombe kali ili
waje kufanya fujo katika mikutano
yetu lengo lao wanataka kuharibu
uchaguzi mzima,” alisema Bw.
Lusinde.
Alimgeukia Bw. Mbowe
akidai amekuwa akijiita yeye ni
mpambanaji mbele ya vijana wa
Chadema wilayani Arumeru na
huku anaishi kwa kutegemea mali
za urithi wa wazazi wake.
Bw.,Lusinde alikanusha vikali
kuwa amefukuzwa kwa kufanya
kampeni kwa kutumia maneno
makali anayoyazungumza katika
majukwaa ya kampeni.
Kwa upande wake mgombea
ubunge kwa tiketi ya chama hicho,
Bw. Sioi Sumari, aliwaahidi
wakazi wa Njeku kuwa endapo
watamchagua atahakikisha anatatua
kero zinazowakabili katika kijiji.
Wakati huo huo, Bw. Mbowe
amesema mafisadi wa CCM katika
uchaguzi wa Jimbo la Arumeru
Mashariki watapigwa mateke ya
kura mchana saa sita.
Kauli hiyo imetolewa na Bw.
Mbowe wakati akihutubia mkutano
wa kampeni katika Kijiji cha
Ngongongare. Alisema mafisadi wa
CCM waliopo Arumeru Mashariki
wataumbuka kwani Chadema
imejidhatiti katika kura.
Aliongeza kuwa mafisadi hao
wanashinda kwa kuiba kura na
kutumia mabavu hali ambayo
inaonesha wazi kuwa wanaiba
demokrasia ya Watanzania.
"Hapa Arumeru Mashariki
Mafisadi wataambulia patupu kwa
kuwa kila kijana na mpiga kura
atalinda kura yake na baadaye
tutahakikisha tunamkesha sasa
hawa mafisadi ambao wanasubiri
kila mara tukalale na kisha wanaiba
kura zetu wataanzaje nawaonea
huruma,” alisema Bw. Mbowe.
Naye mgombea ubunge kupitia
chama hicho, Bw Joshua Nassari
aliwataka wananchi wa jimbo hilo
la Arumeru Mashariki kuachana na
Propaganda ambazo zinaendelea
kuenezwa kuhusu maisha yake.
Wakati huo huo, habari ambazo
gazeti hili limezipata wakati
likienda mitamboni, zilieleza kuwa
kigogo mmoja wa CCM alikamatwa
akidaiwa kugawa rushwa. Taarifa
hizo zilieleza kuwa tukio hilo
lilivuta hisia za wingi, na kuamua
kufuatilia suala hilo kwa kina.
Wakati huo wafuasi wawili wa
Chadema katika Jimbo la Arumeru
Mashariki wametekwa nyara na
watu wasiojulikana, huku mmoja
kuibiwa gari na mwigine akiwa
ajulikani alipo kwa siku ya nne
sasa
Akithibitisha kutokea kwa
matukio hayo Kamanda wa Polis
Mkoa wa Arusha, Bw. Thobias
Andengenye, alisema mtu wa
kwanza ambaye amemtaja kuwa
ni Bw. Ally Juma (32) mkazi
wa Tengeru alitekwa na watu
wasiojulikana na kisha kuumizwa
vibaya.
Bw. Andengenye alisema kuwa
tukio hilo lilitokea juzi saa mbili
za usiku, ambapo watu wanne
walimchukua Bw. Ally na kisha
kumuomba wampeleke katika eneo
la Makumira ambapo alikubali
kutokana na makubaliano ambayo
walifikia.
Alifafanua kuwa mara baada ya
makubaliano hayo aliwapeleka,
lakini ghafla watu hao walimtaka
awashushe ili mmoja ateremke
kabla hajafika Makumira.
"Dereva huyo alipokuwa
akisimamisha gari ili mtu huyo
ashuke ghafla alikabwa na kupigwa
na kitu kizito katika paji la uso,”
alisema Bw. Andengenye.
Alisema watu hao walitoweka
na gari. Alisema mara baada ya
wasamaria wema kutokea walimpa
kijana huyo msaada na kisha
kumpeleka katika hospitali ya
wilaya ambapo hadi sasa anaendelea
na matibabu.
Watu hao waliondoka na gari
aina ya T 563 BTM rangi ya
Peal Wanted ndogo. Mtu huyo
aliyeporwa gari inadaiwa kuwa
mfuasi wa Chadema.
Katika hatua nyingine mfuasi
mmoja wa Chadema aliyefahamika
kama Bw. Omary Abdul, mkazi wa
Sakina jijini Arusha naye amepotea
katika mazingira ya kutatanisha
ambapo hadi sasa hajulikani alipo.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu
na Bw Omary, ambaye ni Bw Christ
Mbajo, alisema kuwa rafiki yake
hapo awali alikuwa na ugomvi na
kiongozi wa CCM (jina tunalo) kwa
kuvaa vazi linalofanana na yale ya
Chadema.
Bw Mbajo alisema kuwa rafiki
yake huyo alitoka katika mkutano
wa kampeni katika eneo la
Ngarasero ambapo alielekea katika
viwanja vya Triple A jijini Arusha
ambapo mara baada ya kufika ndipo
alikutana na kada huyo wa CCM
aliyemtaka avue mavazi hayo.

16 comments:

  1. Mh. LUSINDE, UZUNGUMZAPO ARUMERU UTAMBUE KUWA UMMA WA NCHI UNAKUPATA KUPITIA MAWASILIANO YA KISASA (KWA RADIO,TV, MAGAZETI, KWA MDOMO N.K.) HIVYO CHUNGA UNAYOSEMA. KWA SASA WATANZANIA WAMESOMA NA NI WAELEWA SANA. WATAKUUMBUA!

    MBOWE ATUPE HIZO MALI ZA URITHI? KWA HILI, WANA WA ARUMERU NA WATANZANIA WATAKUCHEKA. INAONYESHA ULIVYO. WANANCHI UNAOWAWAKILISHA HUKO DODOMA WANA SHIDA SANA.

    ReplyDelete
  2. Ndugu zangu watanzania tatizo la huyu bwana mdogo lusinde nikulopoka na kufanya siasa za chuki. hivi wewe lusinde, una akili timamu au ni upumbavu na ushenzi ndiyo vime kujaa. Kwahiyo ulitaka hizo mali za mbowe za urithi ampe mama yako? bora na nina furahi kwa kuwafahamisha watanzania kuwa mali za mbowe ni za urithi.(thanks)haya sasa tueleze za ridhiwani,mkapa,chenge nma wengineo wengi ktk serikali ya ccm

    ReplyDelete
  3. lUSINDE SI MJINGA TU HUKO JIMBONI KWAKE ANAFANYA NINI.hAWA CCM WAMESHATUCHOSHA NASEMA.sASA MH.MBOWE MALI YA URITHI NI KOSA GANI??NINYI CCM MMEZOEA KUIBA,UFISADI MNAJIFANYA MALI ZENU KUMBE MALI ZA WATANZANIA,AFADHALIMH.MBOWE MALI YA URITHI.TOA SERA ZA CHAMA CHAKO SIYO KUZUNGUMZA KAMA MLEVI WA KOMONI.WEWE MALI ZA UFISADI WAJIFANYA NI ZAKO.WAKATI UMEWAFISADI WATANZANIA.MUULIZE RIRWAN.ACHA UJINGA.TOA SERA.MH MBOWE ATACHUWA NCHI SIKU WAJA.UNADHANI WATANZANIA NI WA ENZI ZILE? WE ULIYE TU KULENI VYA MWISHO,2015 MTAONA NA WOTE MTAISHIA JELA.

    ReplyDelete
  4. Hawa jamaa wa CCM wameishiwa sera kwa kuwa hawana jipya la kuwaeleza wananchi wakawaelewa. Kilichobaki kwao ni kutukana na kulazimisha matokeo. siku wananchi wote watakapozinduka hawatakuwa na pa kushika, na siku yenyewe yaja.

    ReplyDelete
  5. Mbwa wa Kichaga wamevamia Arumeru,ole wenu Arumeru mmesahau yale ya Diocese. hao ni nyama hao kwao ni pesa kwanzaa halafu baadaye mengine . wamedhamiria kuchukua nchi kwa udi na uvumba,lakini baadaye mtawaona watakavyowageuka. Huyo Mbowe na Ndesamburo na Mtei ni wahujumu uchumi wa nchi hii waliojificha kwenye mgongo wa siasa kuficha madhambi yao. Mnasherehekea helikopta na kampeni zinazofanyika Arumeru huku wenyewe mkiwa na njaa kali,hamtawaona tena hao wakishapata kura,

    ReplyDelete
    Replies
    1. unamawazo finyu kaka jipange upya ....................siajapo wewe ni mtoto wa kigogooooooooooooooo

      Delete
    2. we kweli huna akila kabisaaaa,kweli nakwambia,

      Delete
    3. Na wewe mtoto wa Mbowe? WACHAGA WEZI NA SLAA KAZUNGUKWA NA WEZI

      Delete
  6. Afadhali Chadema kuliko majambazi ya CCM, ukiwasiliza chadema wanaeleweka siyo CCM wanatunganya mchana kweupe na hali halisi inaonekana. Njaa tuliyonayo na umaskini unaotuzunguka umesababishwa na wizi unaofanywa na hili genge linaloitwa CCM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fanya kazi wewe unategemea Slaa akupe chakula bure? kazi na kujituma kutakuondoa kwenye umasikini

      Delete
  7. Kuwa na mali za urithi si dhambi,bali kuwa na mali za wizi na ufisadi ndiyo dhambi.Mbona CCM hawasemi mali zao za ufisadi?.Kinachowafanya CCM kuhaha wanajua chama cho chote kikiingia madarakani, mafisadi watakosa amani ya kutumia mali zao.Tanzania bila CCM amani itaendelea kuwepo.Wenye haki wanasema hakuna amani kwa waovu.Mafisadi hawawezi kuwa na amani daima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa hii ndio kuishiwa sera,ukweli ni kwamba ccm imechoka tunasubiri muda tu itaanguka
      sas kwani ye alitaka mali za urith afanye aje?

      Delete
  8. Nadhani wanachi wamekuwa na upeo wa ina yake katika kipindi hiki cha mapiduzi ya haki na demokrasia ya haki ya MTU MWENYEWE.Haya mabadiliko ya Nguvu ya Umma hayataletwa na chama chochote bali na wanachi wenyewe. Ni wakati mwingine ambapo Afrika iko kwenye Trasmission Period ya mabadiliko. Napenda kuwapongezasana sana CHADEMA kwa kuliona hilo na kulisomea alama zake ili mapinduzi ya kweli yapatikane. Nawaomba sana hapo Arumeru Mashariki kuwa makini sana na Hatakama chama tawala kitashinda ila ukweli ni kwamba mwisho wa chama tawala unakaribia. TUNAITAJI MABADILIKO. GAMA

    ReplyDelete
  9. Mafisadi na chama chao cha ccm wanajua fika kuwa Chadema watachukua dola kama Usalama na polisi wasipoingilia.Kinachowasaidia ccm ni kwamba chama hiki kinalindwa na usalama wa taifa na polisi,lakini itafika mwisho.Maana usalama na polisi hawatendi haki kabisa.Lakini sisi tunatumia akili na tunamwomba Mungu wao wanategemea mali na vyeo vyao. Nawaimbia hivi siku yaja hakuna cha usalama wa taifa hakuna cha polisi.Nguvu ya umma.Kumbuka Tunisia,Libya na kwingineko ambako mageuzi yamefanyika.CCM inakufa na kuzikwa na kusahauliwa.Na mafisadi wote jela.Ndo maana wanahaha wakijua chadema wakichukua dola basi mwisho wao.

    ReplyDelete
  10. Yeah OK. Inanonesha ni kwa jinsi gani CCM tunaena kuizika. Kwani hawana cha kujitetea lakini wanataka kuchafua watu, ila wanashindwa coz facts zipo,kuwa wao ni WEZI.

    ReplyDelete
  11. HONGERA ARUMERU MASHARIKI KWA KUFANYA KWELI.MMEFANYA JAMBO AMBALO LIMEWASISIMUA WATANZANIA WOTE WENYE AKILI NA WAPENDA MAENDELEO.MUNGU ATUBARIKI NA AENDELEE KUTUKOMBOA KUTOKA KWENYE MAKUCHA YA MAFISADI.MH.MBOWE,MH.SILAA PAMOJA NA KIKOSI KIZIMA CHA KUPIGANIA UKOMBOZI KIPEKEE NAWAPONGEZA SANA NA MUNGU AWALINDE NA KUWATANGULIA KATIKA MAPAMBANO HAYA.MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete