21 March 2012

Kamati ya Bunge yabaini ufisadi

Na Martha Fataely, Monduli


Inatoka uk. 1
“Haya yaliyobainika kwa siku ya kwanza ya
ziara ya kamati ya bunge ni matunda ya uozo
wa muda mrefu‚ mmekuja kutukamua jipu
letu, endeleeni kutukamua ili usaha uliotujaa
umalizike lakini pia itatusaidia tutapona na
kuondokana na tatizo” alisema.
Kuhusu matumizi mabaya ya fedha
yanayosababishwa na kutokupelekwa
kwa vitabu vya ukusanyaji wa fedha za
halmashauri, mkuu huyo wa wilaya alisema
kuna kesi mahakamani dhidi ya watumishi
ambao wamekaidi kupeleka vitabu hivyo.
Kwa upande wake, Mkaguzi wa Hesabu
Kanda ya Kaskazini kutoka ofisi ya CAG,
Bw Swalehe Kiupi, alisema vitabu vya
halmashauri hiyo havioneshi madeni ya
halmashauri hiyo yenye thamani ya sh.
milioni 439.3 hali inayoashiria uwezekano
na kutolipwa.
Alisema halmashauri hiyo imekuwa
ikipata hati zenye mashaka kuanzia mwaka
2007/2011 kutokana na watendaji wake
kushindwa kujibu hoja za ukaguzi katika
miradi mbalimbali ikiwamo ukusanyaji
mbaya wa fedha katika vyanzo mbalimbali.
“Mfano hai ni katika vitabu 24 vya
ukusanyaji wa mapato ambapo kati
yake, vitabu nane vimerudi bila fedha
huku waliohusika katika shughuli hizo
wakifahamika, hii inaashiria usimamizi
mbovu wa vyanzo vyake vya mapato”
alisema.
Mapema mbunge wa Mbozi Mashariki,Bw
Godfrey Zambi alisema taarifa za miradi
ya ukarabati wa barabara ina upungufu
mwingi akatolea mfano wa sh. milioni
372 zilizopokelewa mwaka 2009/2010,
lakini katika mchanganuo wa matumizi
zimeonekana zimetumika sh. mil. 359 bila
kuonesha salio lililobaki.

2 comments:

  1. Tumechoka kusoma mambo ya Uozo wa Halmashauri nchini. Mpaka fedha za halmashauri zikombwe zote ndio Serikali na Bunge zitachukua hatua?

    ReplyDelete
  2. Ukweli hizi ripoti za kila mwaka zinatia kinyaa hakuna utekelezaji imebaki siasa tu mbona hatuoni hatua madhubuti zikichukuliwa kwa wote wanaohusika badala yake ni taarifa taarifa hazitusaidii hata kidogo.

    ReplyDelete