03 February 2012

Wachinjaji wa nyama Vingunguti wagoma kuchinja nyama

Na Flora Amon.

WACHINJA  nyama zaidi ya mia mbili wa machinjio ya vingunguti  iliyopo Ilala jana wamegoma kuchinjisha wanyama wao kwa madai ya kuchoshwa na ufisadi unaofanywa na mhasibu wa machinjio hiyo.

Wakizungumza na Majira wa nyakati tofauti Dar es Salaam jana,mmoja wa wadau wa wachinjaji nyama Bi.Rehema Hassan,alisema Mhasibu huyo amekuwa akishindwa kuwapa risiti pindi wanapohitaji kunjisha wanyama wao toka mwaka 2010.

Alisema kwakukosa haki zao za msingi kipindi ng'ombe anapopotea hawaezi kulipwa kwakuwa hawana risiti ndipo walipokutana wadau na kujadiliana ndipo muhafaka ukifikia kuwa wawe wanapewa risiti ili hata ng'ombe hakipotea waweze kulipwa.stakadhi zao.

Aliongeza kuwa makubalianao hayo yalitakiwa kuanza jumatatu lakini mhasibu akawa ajizungusha ambapo juzi akaanza kutoka risiti lakini kwa muda mbaya.

"Tulikubaliana saa 12.00 jioni awe ameanza kutoa risiti na kuhesabu ng'ombe lakini yeye saa 12.30 ndiyo alianza kazi hiyo mpaka saa 8 usiku risitizikawa zimemuishia na ng'ombe wengine hawapiliwa"alisema Bi.Hassan.

Alisema mhasibu huyo amekuwa akipunguza idadi ya ng'ombe ambapo ukimpa kama elfu kumi kwa ng'ombe  wanne yeye kwenye risiti anakuandikia ng'ombe wawili hali ambayo inazusha mgogoro kwa mtu anayechinja akadai kufuata risiti ilivyoandikwa.

"Unajuwa ng'ombe mmoja kushinjisha ni sh.2500 sasa mhasibu jana baada ya kumsumbua risiti ameanza mtindo mpya unamuonyesha kuwa una ng'ombne watano na unalipia hela lakini yeye kwenye risiti anaandika pungufu,sasa mchinjaji yeye anagoma kuchinja kwa madai yakufuata risiti ilivyoandikwa na sisi tukasema hatuwezi kuchinja wanayama nusunusu vinginevyo tunagoma ndiyo tumegoma"aliongeza.

Kwa upande wa Ofisa mfawidhi wa machinjio hiyo Bw.Juma Nganyanga alikiri kuwepo kwa mapungufu kwa mhasibu huyo ambapo alisema tayari ameondolewa asubuhi toke kutokea kwa vurugu hizo na kuna mhasibu mwingine kutoka Ukonga anaanza kazi rasmi.

"Kuhusu kutopewa risiti ni kweli mpaka mimi nikawa kila siku namsisitizia atoe risiti,kwani kulikuwa na kunakushindana na mimi lakini,ila baada ya vuruvu kuchukuliwa kwenda ofisini kwa ajili ya mahojiano na ameletwa mhasibu mwingine toka Ukonga"alisema Bw. Nganyanga.

Kuhusu na yeye kukataliwa na wachinjishaji hao alisema kuwa yeye anafuata sheria kma vile kupiga marufu uchinjwaji wa vibudu na wachinjishaji kuwa wasafi ndiyo maana wananchukia kutokana na kuwabana na sheria.

Naye Kaimu Ofisa wa Kilimo cha mifugo Dkt.Audifas Sarimbo aliyefika kutoa suruhisho kwa  niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa Ilaa,aliwasasihi wachinjisaji hao kutoendele na mgomo kwani mhasibu ameshaondelewa na wataongezewa mwingine wa pili ili kurahisha kazi.

Alisema kweli swala la rushwa litakuwepo lakini wanaendelea kufuatili na huku wakiendele kumuhoji mhasibu kwa tuhuma zinazomkabili.


No comments:

Post a Comment