03 February 2012

RAIS Jakaya Kikwete amewashauri wawekezaji kuwekeza kwenye kilimo

Pamoja na mabenki kutokana na kwamba Tanzania inayomazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na ardhi yenye rutuba mzuri.

Rais aliyasema hayo Dar es Salaam jana, wakati akizindua benki mpya ya First Nation Benk (FNB), ambapo aliwataka wawekezaji kuhakikisha wanawekeza nchini hapa ambapo alisema kuwa kufanya hivyo kutaweza kuongeza tija kwa Taifa na jamii kwa ujumla.

"Sekta za fedha zimekuwa zikifanikiwa hapa nchini kutokana na mazingira mazuri yaliyopo hivyo ninawashauri kuendelea kufanya hivyo ili kuongeza tija na ufanisi katika nchi yetu," alisema Rais Kikwete.

Aidha alisema asilimia 70 ya watanzania wengi wanajishughulisha na shughuli za kilimo na hii ni kutokana na kwmba kina ongeza nguvu kazi na uzalishaji.

"Napenda kusema kuwa huduma mzuri katika mabenki inahitajika zaidi ili kuweka kukuza uchumi wa nchi kupitia mabenki haya na pia itasaidia kuleta mabadiliko makubwa ndani na nje ya nchi," alisema na kuongeza,

"Ninawahakikishia kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano mzuri katika kuhakikisha jitihada zinazofanywa zinafanikiwa zaidi na pia wengine kuiga mfano wa kuja kuwekeza hapa kwetu," alisema.

Rais Kikwete alisema kuwa hadi sasa benki 47 za watu binafsi zimewekeza hapa nchini ikijumuishwa na FNB hivyo kufanya soko la tanzania kuendelea kukua na ndio maana nchi hii inasherehekea, na kwamba benki zinafanya vizuri na pamoja na biashara zinazofanyika ni mzuri'

Pamoja na kwamba kuna ushindani kati ya mabenki na wateja, Tanzania Mortagage Refinancing Company(TMRS) imeweza kuwa na ushirikiano kutoka Azania Banki, Tanzania Investment Bank, Exim Bank, CRDB Bank, National Micro-finance Bank, Dar es Salaama Community Bank na  Banc ABC hivyo sina shaka kwamba FNB itakuwa ni moja ya wawekezaji wake.

Hata hivyo aliutaka uongozi kufanya ushawishi wa hali na mali kwa kuwashawishi wananchi ili waweze kujiunga katika benki hiyo.

"Tunashukuru South Afrika kwa kutudhamini na kutambua umuhimu wa nchi yetu hivyo kufanya maamuzi ya kuwekeza Tanzania na hii ni kutokana na kuona umuhimu wa Sekta Binafsi katika nchi nyingi ikiwamo nchini hapa," alisema. 

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Bi. Elizabeti Nyambibo, alisema kuwa uzinduzi wa benki hiyo umekuja kutokana na mausiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

"Kuwapo kwa benki hii ni moja ya mafanikio makubwa katika nchi yetu na hii ni kutokana na ushirikiano wetu na nchi hii na pia itatujengea mahusiano mazuri na nchi zingine kama tulioupata kwa nchi hii," alisema Bi. Nyambibo.

No comments:

Post a Comment