LUSAKA, Zambia
RAIS wa Zambia, Michael Sata amemteua Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Chishimba Kambwili, kumwakilisha katika hafla ya kufunga michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Jumapili ijayo mjini Libreville, Gabon.
Rais Sata alipewa mwaliko na Rais mwenzake wa Gabon, Ali Odimba Bongo kuhudhuria hafla hiyo ya kufunga michuano hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Ikulu mjini Lusaka na Ofisa Habari, George Chellah rais huyo hataweza kuhudhuria fainali hiyo na badala yake amemteua Waziri wa Vijana na Michezo, kumwakilisha katika tukio hilo muhimu.
Vilevile kupitia taarifa hiyo, rais huyo aliipongeza timu ya taifa ya Zambia 'Chipolopolo' kwa kufika hatua ya nusu fainali, baada ya kulilaza Sudan kwa mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment