08 February 2012

Ghana yakiri kusonga mbele kwa bahati

Ghana yakiri kutinga kwa bahati

BATA, Equatorial Guinea

TIMU ya taifa ya Ghana, imekiri kwamba ina bahati kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika, baada ya kuzawadiwa ushindi na Tunisia katika mechi ya robo fainali.

Katika mchezo huo wa Jumpili, timu zote zilikuwa zimetoshana nguvu hadi kipa wa Tunisia, Aymen Mahtlouthi aliposhindwa kuzuia kombora lililoelekezwa langoni kwake na Andre 'Dede' Ayew na kuifanya timu hiyo, ipate ushindi wa mabao 2-1.

"Nadhani tuna bahati," alisema mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan, mara baada ya mechi hiyo.

"Unafahamu katika soka kila kitu kinaweza kutokea, bahati nayo inaweza kutokea na unaona makosa aliyoyafanya mlinda mlango," aliongeza nyota huyo.

Hata hivyo alisema hawezi kulaumiwa, lakini hali hiyo ndiyo iliyojitokeza.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kukiri huko kwa Gyan, kumekuja baada ya pia kuonekana jinsi Black Stars, ilivyocheza katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Botswana, huku timu hiyo ambayo inapewa nafasi ya kutwaa ubingwa, ikifanikiwa kushinda mechi tatu na kutoka sare moja bila kufikia kiwango cha juu.


No comments:

Post a Comment