PERU,
WAPELELEZI wameambiwa
waliache kabila linaloishi maisha yao porini kama ya wahadzabe wa Tanzania,
walio katika bonde la mto Amazon.
Wito huo huyo umetolewa
baada ya kutolewa picha ya wanafamilia kwenye mtandao.
Walipigwa picha mwaka jana
na mtafiti wa historia ya binadamu na makabila na habari kutolewa katika
mtandao wa Survival International .
Lakini Mariela Huacchillo,
wa ofisi ya inayoshughulika na ulinzi wa Maeneo ya asili alionya kutokaribina
na watu hao kitu ambacho kinaweza kusababisha kuambukizwa virusi hatari ambazo
haviko katika maeneo yao na wenyeji hao wanaweza kukasirika.
Huacchillo aliwataka watu wanaokwenda
kutojaribu kugusana na jamii hiyo ambayo inajaribu kuwa nje ya dunia.
Aliwatakja watu wanakwenda
katika eneo hilo kutowaachia chakula, nguo au zawadi nyingine kwa lengo la kwua
karibu nao.
Oktoba mwindaji mmoja
alijeruhiwa na mshale butu uliofyatuliwa na mmoja wa wawindaji wa kabila hilo.
Tukio kama hilo
liliripotiwa mwaka 2010, ambapo kijana mmoja alipigwa mshale na kujeruhiwa.
Taasisi ya Survival
International ilielezea kifo kilichotokea mwaka jana cha Nicolas
"Shaco" Flores, ambaye alikuwa akiwapelekea chakula na zawadi
nyingine kwa miaka 20 watu hao ambaye alipigwa mshale na watu wengine
wasiomfahamu.
Tukio hilo
halikuthibitishwa.
Kuna kama makundi 15 ya
watu wanaishi msituni yasiyofahamiana katika msitu wa Amazon nchini
Peru, kwa mujibu wa taarifa
ya serikali.
Kumekuwa na wapelelezi
wanakwenda katika maeneo hayo kwa helikopta kwenye miaradi ya mafuta na gesi
kwenye misitu hiyo kitu ambacho kinawafanya watu hao wanaoishi mstuni
kutawanyika, wanasema wanaharakati.

No comments:
Post a Comment