STOLKHOM,
PACHA waliozaliwa Indonesia
na kutenganishwa baada ya kuasiliwa wamekutana baada ya kutafutana ambapo
walikwua wakiishi katika eneo la karibu kiasi cha kilometa 40, kusini mwa
Sweden, baada ya kupita miaka 30.
Emilie Falk na Lin Backman
walikuwa wakiishi mbalimbali kwa miaka 29 na waliungana mwaka uliopita.
Kipimo cha vinasaba DNA
ndicho kilichobainisha udugu wa wawili hao Januari mwaka jana, kwa mujibu wa
AFP kuna asilimia 99.98 kwamba ni ndugu.
Kuna baadhi ya mambo
yaliyofuatia hadi kuja kubainisha ukweli huo.
Wote wawili walikuwa
wameasiliwa katika kituo cha watoto yatima Semarang kaskazini mwa Indonesia na
wapenzi wa wenye asili ya Sweden, lakini hakukuwa na nyaraka rasmi za kuonyesha
kuwa walikuwa pacha.
Wakati wazazi wa Backman
waliacha nyaraka zote miaka hiyo kwa dereva taksi ambaye alikuwa ni baba yao.
Majina hayo yalisaidia
wazazi wa Backman kumsaka Falks nchini Sweden, familia hizo zilikutana mara
chache wakati pacha hao wasichana wakiwa wadogo ili kuangalia majina.
Nyaraka za umilikishwaji
hazikuwa na vielezo vya kutosha kuonyesha ni ndugu lakini kipimo cha DNA ndicho
kilithibitisha ukweli alisema," Falk.
Kitu kingine
kilichowachanganya ni utofauti wa majina ya ubini, ingawa jina la mama yao
lilikuwa ni moja.
Falk alisema kutokana na
utata uwezekano wao ni ndugu walijaribu kusahau lakini aliwaza kumtafuta mwenzi
na kujua uweli baada ya kuelewa miaka miwiwli iliyopita.
Alianza kufikiria kuhusu
familia yake na alivyoasiliwa baada ya kuolewa miaka miwili iliyopita,
alipomuuliza mama yake alimweleza tena kuhusu stori hiyo na akaanz akumtafuta
Lin," Falk alisema.
Alipata jina lake na kuanz
akulitafuta kwenye mtandao akiulizi mtoto wa ki-Indonesia aliyeasiliwa na
familia ya kiswedeni ndipo alimpata kwa kutumia
Facebook.
"Nilizaliwa Machi 18,
1983 Semarang na mama yangu mzazi ni
jina lake ni Maryati Rajiman," Falk alisema kuwa alikwua ameandika hivyo,
na kisha alijibiwa: "
Pia na mimi huyo ni mama
yangu! na tarehe hiyo ndiyo niliyozaliwa!"
Walikuja kufundua kuwa na
vitu vinavyofanana.
Walikuwa wakiishi katika
eneo ambalo linatengwa na umbalia wa kilometa 30 huku wote wakiwa ni walimu,
walikuwa wameolewa siku moja katika mwaka tofauti na hata wimbo wao wa harusi
ulikuwa mmoja wa "You and Me" ulioinbwa na Lifehouse.
"ILikuwa ni kitu cha
kustajabisha," Falk alisema.
"Wakati Lin
aliponiita (akwia na majibu ya DNA), nilikumbuka nilikuwa nimekaa katika
gari wakati alipniambia na kuanza kucheka kwa kwua niliona ni kitu cha
ajabu," alisema na kuongeza:
"Kisha nilianza kusikiria kuhusu kulala katika tumbo moja.
Kuanzia wakati huo wawili
hao wamekuwa karibu wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara kwa simu na
wanazungumzia kuhusu kurejea Indonesia kuwasaka wazazi wao wa damu.
Baadhi ya nyaraka za mabinti
hao zinaonyesha kwua baba yao alikwua dereva teksi.
Falk anasema ingawa
anatamani wangejuana mapema zaizi lakini hasikitiki kuhusu kitu ambacho hakujua
na kwamba naafuarahi kwa kukutana na ndugu yake.

No comments:
Post a Comment