CAPE TOWN
NYANI wa walioa katika
hifadhi ya Cape Point nje ya jiji la Cape Town, Afrika Kusini wamekuwa wakileta
usumbukwa watalii ambapo wana uwezo hata wa kufungua milango ya magari.
Gari linaposimama nyani
hayo huenda katika milango ambao kama itakuwa imesahalika kuwekwa kizuizi ndani
huweza kufungua ili kuangalia kama kuna chakula.
Nyani kama hao pia wamekuwa
wakileta usumbufu katika mpaka kati ya Zimbabwe na Zambia ambapo huvamia magari
ili kupata chakula.
"Nyani ni tatizo
ambalo linatakiwa kushughulikiwa wanaponguza wageni kwa kutaka kupora
vitu," Meneja wa Kituo cha forodha cha Zimbabwe katika mpaka wa Chirundu ,
Tichaona Phiri, alialiambia gazeti.
"Wakati mwingine
hungata au kupiga watu usoni kama watajaribu kuzuia vitu vyao na wanaweza
kuwapora mabegi wanawake na hata kufanya uharibifu wakati wakisaka chakula kwa
gari."
Wakati mwingine hupafua
magunia ya mahindi kwenye malori yanayopita kwenye mpaka, Kamati ya bunge
iliambia baada ya kutembelea hifadhi.
"Nyani hawa wanaweza
kunusa harufu ya mahindi kwenye na kufikiri kuwa kuna kiasi kikubwa, ni ngumu
sana kuwadhibiti," gazeti lilimkariri Phiri akisema.
"Lakini tatizo ni
kwamba wamekwua na tabia kama binadamu na wamekuwa na mbinu," alisema Phiri.

No comments:
Post a Comment