02 February 2012

WANAFUNZI WA CHUO WABADILISHANA MAWAZO.

Na David John.

JUMLA ya wanafunzi 41 wa Elimu ya juu waliomaliza katika Chuo kikuu cha Massacheser  Institute of Technoloji (MIT) kilichopo Marekani wamekutana na wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchi  kwa lengo la kubadilishana mawazo, na uzoefu,katika kukuza ujasiriamali  na hasa katika nyanja ya mfumo wa Teknohama.

Akizungumzia  mwaliko huo Dar es salaam jana  Ofisa Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator  (ICT) Bw. George Mulaba alisema kuwa Tanzania Commisioni For Science na Teknoloji kupitia tasisi yake ya COSTERCH wamewaalika wahitimu hao wa mastar kutoka marekani ili kuja kubalishana na kupeana mawazo , kuhusiana na Ujasiriamali na mambo ya Tecknohama.

Alisema wanafunzi hao 41 wamekutana na wanafunzi wezao 71 waliomaliza katika vyuo mbalimbali nchini na wale ambao bado wako vyuoni ilikuweza kuona namna gani wanapeana changamoto, mbinu pamoja na kukabiliana na matumizi ya Tekinolojia ya kisasa .

"wanafunzi hao ni Graduete ngazi ya mastera sasa wamekuja ili kutoa changamoto kwa wezao na kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea baada ya kumaliza masomo yao"alisema Bw. Mulaba

Alisema vijana wengi wanapo maliza masomo wanakosa mawazo mapya na kutegemea kupata ajira  kumbe kuna mbin zingine za ujasiriamali na kama wanapata changamoto fulani wanaweza kuendesha maisha yao bila kutegemea ajira.

Alisema kwa kutambua hilo wameamua kuwaunganisha na wezao ambao ni vijana kutoka nje ya nchi  waliojikita katika ujasiriamali na kwakufanya hivyo vijana wandani watapata fursa ya kupata mawazo mapya.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Hassan Mshindo. alisema lengo la kuwaleta vijana hao waweze kuwapa changamoto vijana wandani ili wafikie mahali waweze kujiajiri wenyewe bila kutegemea ajira.

Aliongeza kuwa mbali na kubadilishana mawzo lakini watatumia fursa hiyo kuweza kutengeneza mazingira ya kukuza makampuni yao, na katika hilo lazima waweze kuwa na ushirikiano na wezao kutoka nje ya nchi.

"Nachotegemea sasa vijana hawa kupitia changamoto ya wezao wataweza kukuza ujasiriamali, ubunifu, utakao wafanya kufanya kazi zao binafsi."alisema Dkt. Mshindo.

Alisema Tasisi hiyo mbali na kuchukua vijana waliomaliza vyuo vikuu lakini pia wanachukua hata wale ambao wana Certificate na hivi sasa wanaanda mfuko malumu utakaoweza kuwasaidia vijana wasiokuwa na uwezo ili waweze kupata ubunifu, na baadae waweze kujiari wenyewe. 





























No comments:

Post a Comment