Watendaji wakuu wa serikali hasa katika ngazi ya kitaifa.
Rushwa hiyo kubwa ina athari kubwa katika masuala ya kisiasa,kiuchumi na ni tishio kwa utengamano wa kijamii na umoja wa kitaifa.
Vilevile rushwa ya aina hii inahusisha uporaji wa rasilimali za nchi na wakati mwingine kutoroshwa nje ya nchi.
Hali hii inadhoofisha kwa kiasi kikubwa harakati za kujenga jamii huru na inayoendeshwa kwa misingi bora ya kidemokrasia.
Pia vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu ambavyo vimekithiri duniani na hata hapa nchini vinatokana na kushindwa kwa harakati za wanyonge kuupindua mfumo wa ubepari wa kibeberu.
Hata hivyo harakati hizo bado zinaendelea duniani kote na huenda zikachukua muda mrefu zaidi kutokana na kuwepo kwa uwezo wa kijeshi na kifedha wa dola zinazodhibitiwa na watu wachache wanaonufaika na mfumo huo.
Vita dhidi ya ufisadi ni vita halali dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa sababu vinalenga kulinda rasilimali muhimu za kuiwezesha serikali kumudu gharama za kulinda haki za binadamu na kujenga demokrasia.
Chimbuko la ufisadi nchini Tanzania ambalo lina manufaa kwa watu wachache wenye nia ya kuunyonya umma ndiyo kichocheo kikuu cha kuwepo kwa uvunjifu wa haki za binadamu.
Historia ya vita dhidi ya ufisadi.
Historia dhidi ya ufisadi nchini Tanzania inaweza kugawanywa katika vipindi vikuu viwili ambavyo ni kipindi cha siasa ya ujamaana kujitegemea (1967-1985) na kipindi cha uliberali mambo leo (1985 hadi sasa).
Katika miaka 24 ya utawala wa awamu ya mianya ya ufisadi ilizibwa ingawa vitendo vidogo vya rushwa na hongo vilikuwepo.
Kuanzia mwaka 1967 chama cha TANU kilitangaza vita dhidi ya mifumo ya kifisadi kupitia azimio la Arusha ambapo pia chama hicho kilianisha aina ya nchi inayokusudia kuijenga.
Vilevile TANU kupitia azimio hilo ilitangaza vita kulitoa taifa katika hali ya unyonge na kuwafanya wananchi watoke katika hali ya dhiki.
Kwa wakati huo ili kuwadhibiti viongozi wakuu wa serikali na vishawishi TANU iliweka miiko ya uongozi .
Kwa mujibu wa miiko hiyo kila kiongozi alitakiwa asiwe na hakimkatika kampuni yoyote,mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila ,asiwe na mishahara miwili au zaidi wala nyumba ya kupangisha.
sehemu ya mapambano ya vitendo vya kifisadi ndani ya serikali ya jamii.
Vita hivi vilikuwa vigumu na hatari kwa sababu vilikuwa vita vya nguvu ya hoja na umadhubuti wa silaha.
Itikadi ya ujamaa wa kujitegemea ndiyo ilikuwa nguvu na silaha kali iliyochaguliwa kutumika katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Kwa ujumla TANU ilitangaza vita vya kujenga taifa huru lenye usawa na linalojitegemea.
Hata hivyo kwa bahati mbaya kabla ya TANU haijafanikiwa kuleta mapinduzi ya kuondoa unyonge wa wananchi wa Tanzania mabeberu na vibaraka wao walitumia jasho la wanyonge kulipindua azimio hilo.
Kupinduliwa kwa azimio hilokulisababisha kufungua milango ya mafisadi waliokubuhu.
Baada ya hilo TANU ilitanagaza vita ya ukombozi wa wanyonge bila mkakati wa kuwaandaa wanyonge ili waweze kuwa na ari na nguvu ya kupamabana na kujipatia ushindi.
Kwa hali ilivyokuwa kwenye uwanja wa vita TANU haikuweza kushinda kutokana na ushiriki mdogo wa wanyonge ambao ulisababishwa na mazingira magumu ya kisiasa ya kutokushirikiana baina ya uongozi wa wa juu wa kisiasa na taasisi za ushiriki wa umma.
Hata hivyo baada ya anguko hilo mapinduzi yalifanyika na kufanikisha azinio la Zanzibar kuanzishwa mwaka 1992 ambalo lilidumu kwa muda wa miaka 26 na ulichangia zidi kulitumbukiza taifa katika hali ya unyonge na umasikini .
Hivi sasa katika kipindi hiki cha Uliberali mambo leo (1985 hadi sasa) ufisadi umekuwa janga la kitaifa na kichocheo kikubwa cha vitendo vingi vya uvunjifu wa haki za binadamu.
Kwa mujibu wa Profesa Issa Shivji mfumo huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuasisi sera ambazo utekelezaji wake unaruhusu kuwepo kwa vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa haki za binadamu kwa kiasi kikubwa.
Pia mfumo huo umeasisiwa bila kuwepo kwa mikakati ya kuzuia mianya ya ufisadi na hata juhudi na mbinu ambazo zimekuwa zikifanywa na wapigania haki bado hazijafanikiwa.
Misingi mikuu iliyopo katika kipindi cha sasa ambayo ni ya kifisadi ni uwezeshaji wa wawekezaji kutoka nje ya nchi, dola kujitoa katika shughuli za uchumi ,sekta za huduma za jamii, ulegezaji wa masharti ya soko la fedha, biashara ya nje na ndani kwa maana kwamba serikali haidhibiti tena biashara.
Vilvile ubinafsishaji wa mashirika ya umma,ardhi,misitu,maji,wanyamapori pamoja na huduma za elimu, afya na umeme.
Kwa hali hiyo ni wazi kwamba vita dhidi ya ukiaukaji wa haki za binadamu haiwezi kufanikiwa kwa sababu bado kuna mapambano makali dhidi ya ufisadi
Mbunge wa Same Mashariki Bi. Anna Kilango anasema uwekezaji usiokuwa na tija nao umesababisha ufisadi ambapo viongozi wachache wa nchi zinazoendelea kama Tanzania wamejiingiza katika vitendo vya kifisadi kwa kukosa uzalendo.
Anasema hali hiyo imesababisha watanzania kuishi maisha ya shida na hata kushindwa kutetea haki zao za msingi.
Anaelezea kuwa ili kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa serikali ihakikishe inawachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotumia nafasi zao za uongozi vibaya ikiwa ni pamoja na kuwanyima nafasi za uongozi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka yao vibaya.
Anaitaka serikali kuwa makini na viongozi wasiojali maslai ya taifa na kuendekeza vitendo vya ufisadi kwa sababu vinasababisha ukiukaji wa haki za binadamu.
Anasisitiza kuwa viongozi wote wanaojihusisha na ufisadi wasipewe nafasi za kuongoza na hata ikiwezekana kama wako kwenye madaraka waondolewe.
Anasema mahakama ni lazima zifanye kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa kuhakiksiha kuwa kesi za viongozi wote wanojishughulisha na ufisadi zimashughulikiwa haraka ili kulinda heshima ya utawala bora.
"Ni lazima vitendo vya ufisadi vikomeshwe kwa nguvu zote ili kulinda haki za watanzania wenye kiu ya kufaidi rasilimali za nchi yao," anasema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw.Bashiru Ally anasema pamoja na vitendo vya kifisadi kuwa kichocheo kikubwa cha uvunjifu wa haki za binadmu viongozi wa ngazi za juu ambao ndiyo wahusika wakubwa ni lazima waelewe kwamba ufisadi ni hatari kwa mustakbali wa nchi.
Anasema mabadiliko ni lazima yafanyike kuhakikisha kuwa tatizo ambalo hilo ni la kmfumo linapigwa vita vikali.
Lakini ili kuwa na mafaniko ni lazima iwepo jamii yenye uwezo wa kupiga kelele na kupinga vitendo hivyo.
Anashauri kuwa uwajibikaji ni lazima ufanyike kwa vitendo ikiwa ni pamoja na serikali kusitisha mikataba yote mibovu ambayo haina maslai kwa taifa.
Mikataba hiyo ijadiliwe na kuridhiwa na bunge kabla ya kuanza kwa utekelezaji.
"Tuna mikataba mingi mibovu ambayo ipo kwa ajili ya kuwaumiza wananchi tu na wala haina manufaa yote," anasema.
Wawekezaji wasiruhusiwe kwenda vijijini moja kwa moja kabla hawajapitia kwa mamlaka zinazohusika ambazo ndiyo zenye uwezo wa kutoa mwongozo.
No comments:
Post a Comment