Na Mwandishi Wetu
JESHI la Polisi inawashikilia wafanyabiashara wawili raia wa kigeni kwa kosa la kufanya biashara kwa kutumia mitungi ya gesi mali ya kampuni Tanzania Oxygen Limited (TOL) kinyume na taratibu za kibiashara.
Watuhumiwa hao raia wa Kichina na wamiliki wa kampuni ya gesi ya Chang Ging International Investment, iliopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam wamekamatwa na mitungi ya gesi mali ya TOL na kusambazia wateja gesi ambayo haina kiwango.
Kamanda wa kanda ya Kipolisi Ilala, Ahamed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa raia hao wakigeni, katika tukio liliofanyika Jumatano, wiki hii.
Menaja mauzo TOL Pwani, Bi. Joyce Mmari, akielezea tukio hilo alisema walifanya msako wa kushtukizia na kufanikiwa kupata mitungi 31 iliojaa gesi ambayo imechakachuliwa.
“Gesi yetu tu ndio ina kiwango cha juu (purity 99.9%) kinachokibulika hospitalini, wakati kwenye mitungi iliokamatwa ilikuwa na gesi ya kiwango cha chini ya asilimia 50” alisema Bi. Mmari.
Aidha, Bi. Mmari alisisitiza ya kuwa kutokana na kampuni ya TOL kuwa na gesi ya kiwango cha juu, mitungi yao imekuwa ni kimbilio ya wafanyabiashara wengi wasio waaminifu.
“Tuna sababu nyingi za kiusalama, ni kampuni yetu pekee ina utaratibu wa kukagua mitungi yake kwa ajili ya kujua kama ina nyufa, kufuja na unyevu ili kuzuia milipuko na ajali zinazoepukika,” alisema Bi. Mmari.
Mwezi uliopita katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, mtu mmoja alipoteza maisha baada ya kulipukiwa na gezi na tukio kuripotiwa katika kituo cha polisi cha Kijitonyama.
“Kwenye hii biashara mtaji mkubwa ni mitungi, unaweza ukazalisha gesi kwa wingi lakini ukikosa mitungi ya kusambazia basi biashara yako imedoda,” alisisitiza Bi. Mmari.
Kwa upande wake, Bw. Daudi Mlwale alisema hiyo sio mara ya kwanza kukamata wachina na mitungi ambayo si mali yao.
Kampuni ya TOL ndio wazalishaji wakubwa Tanzania wa gesi ya kabonidioxide kwa matumizi ya viwandani kama vile vya Soda, Bia na hata Maji.
Vilevile ni wazalishaji wa oxygeni ya viwandani na za hospitali, nitrogeni inayotumika kwenye ndege na kutumia kwenye maabara.
No comments:
Post a Comment