01 February 2012

WAATHIRIKA wa mabomu yaliyotokea katika Kambi ya Gongo lamboto

Na Heri Shaaban

WAATHIRIKA wa mabomu yaliyotokea katika Kambi ya Gongo lamboto jana waliandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kupeleka madai yao kwa Serikali baada kuwatelekeza muda mrefu kwa kushindwa kuwajengea nyumba walizowaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa waathirika hao Bw. Obadia Mgidange alisema kuwa wamevamia katika ofisi hizo kutokana na serikali kushindwa kutujengea nyumba walizohaidi na kuwathamini watu waliokumbwa na mafuriko tu.


Bw.Mgidange alisema kuwa awali serikali iliwaahidi kuwajengea nyumba eneo la Kinyerezi lakini wamesubiri muda mrefu bila kuona utekelezaji wowote wala kupewa taarifa walipofikia.

"Leo tumefika kwa Mkuu wa Mkoa tupo zaidi ya 100 ili  kukumbushia madai yetu kutokana na serikali ya mkoa kuwapa kipaumele watu waliokumbwa na mafuriko badala sisi tuliolipukiwana na mabomu"alisema.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Dar es Salaam Bi.Teresia Mbando alisema kuwa kuhusiana na madai yao ofisi yake inalishughulikia pamoja na kuwafanyia tathimini upya kwa wale waliomba.


Bi.Mbando alikili ni kweli serikali imechelewa kuwajengea nyumba wathirika wa Gongolamboto kutokana na  serikali kushitakiwa na wakazi wa Kinyerezi waliokuwa wakiishi eneo hilo ambalo Manispaa ya Ilala ilitaka kupitisha mradi wa viwanja 20000.

"Tulitarajia  kuwajengea nyumba zenu katika mradi wa viwanja 20,000 Kinyerezi lakini sasa hivi tunatarajia kuwapeleka Msongola ndani ya manispaa hiyo kutokana na mgogoro huu," alisema.


Alisema kuwa utaratibu wa ujenzi eneo la Msongola umeshanaza na SUMA JKT ndio wamepewa kazi hiyo na kazi rasmi ya ujenzi unaanza leo.

Kuhusu kodi ya waathirika ambao wamepanga serikali bado inaendela kulipa sh.600,000 kwa ajili ya kodi ya pango mpaka hapo nyumba zao zitakapo kuwa tayari.

Pia alisema kuwa tatizo lililosababisha ucheleweshwaji wa  malipo ya hundi zao  limetokana na mkanganyiko wa majina hata hivyo alihaidi kwamba litashughulikiwa upya.


No comments:

Post a Comment