01 February 2012

VICOBA anzisheni SACCOS mkope-Mbunge

Na Heri Shaaban

UMOJA wa vikundi vya VICOBA katika Kata ya Majohe wilayani Ilala imepata shilingi milioni 3.7 baada ya kufanya harambee juzi jijini Dar es Salaam.


Harambee hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Bi.Eugen Mwaiposa wakati wa kuzindua kikundi hicho.

Akizungumza mara baada kuzindua kikundi hicho Bi.Mwaiposa aliuomba umoja huo wa kuweka na kukopa, wanapokopa fedha wakumbuke marejesho ili waweze kukuza mitaji yao.

"Leo nawachangia sh.milioni 2 katika umoja wenu,nawaomba muunde SACCOS yenu ili muweze kukopa fedha na VICOBA yenu iweze kukua na kuwa na wanachama wengi," alisema Bi.Mwaiposa.

Alitaja fedha zilizopatikana katika harambee hiyo wadau walichangia sh.40,500,wanachama sh.450,000 fedha za papo hapo sh.900,000,na za kucheza muziki sh.54,000 na ahadi sh. 800,000.

Aliwataka waungane katika umoja huo na kuacha kufarakana na kuchagua viongozi waadilifu watakao weza kuongoza benki yao.

Kwa upande wake Katibu wa VICOBA hiyo Bi.Amina Kapundi alisema kuwa umoja wao ulinzishwa mwaka 2009, hadi kufikia mwaka 2012 January kulikuwa na vikundi hai 20.

Bi.Amina alisema kuwa mpaka sasa kuna wanachama hai 449 ambao wanashiriki katika vikundi na kuudhuria semina zao na wananunua hisa vizuri.


No comments:

Post a Comment