01 February 2012

TCRA ya ahidi kufadhili wanafunzi wa ndani

David John na Goodluck Hongo.

 SERIKALI kupitia mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa itaendelea kufadhili wanafunzi wa vyuo vya ndani ili kuendeleza taaluma itolewayo na vyuo vya hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya utoaji ufadhili  kupitia mamlaka ya mawasiliano nchni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Dar es salaam jana Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Profesa John Nkoma alisema kuwa wataendelea kufadhili wanafunzi wa vyuo vya ndani  kwa kuwa ni faida kwa vyuo na kwa wanafunzi wenyewe.

Alisema kuwa mawasiliano (Tehama) ni sekta inayokuwa kwa kasi nchini  na duniani kote hivyo  kunahitajika kuwa na watalamu wa kutosha ili kuweza kuendana na changamoto zilizopo katika mawasiliano.

"Hivi sasa katika sekta ya mawasiliano kumekuwepo na changamoto kubwa  hivyo lazima tuwe na wataalumu wakutosha ili kuweza kukabiliana natatizo la uhaba wa wataalamu nchini."alisema Profesa Nkoma.

Naye Waziri wa Mawasiliano  Sayansi na Teknolojia  Profesa  Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo lakini akiwakilishwa na Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt Florens Turuka  alisema taasisi hiyo ni mala yao ya kwanza kufanya jambo hilo ambalo ni jema na lenye kusudio zuri kwa sekta ya mawasiliano , sayansi na teknolojia.

Aliongeza kuwa vyuo  vya hapa nchini vimekuwa vikijitahidi kufundisha na kutoa watalamu wa zuri wa Tehama lakini suala la idadi ndogo la wahitimu katika Tehama linakwamisha na uhaba wa fedha za kuwasomesha .

 Alisema kuwa pamoja na serikali kuazisha Bodi ya mokopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu ili kufanikisha kwa wahitimu wengi zaidi changamoto kubwa imekuwa katika kukidhi azma ya kuwa hudumia wote wanaotaka mikopo hiyo.

"Nawasihi wote mliopata ufadhili huu kuitukia fursa hiyo vizuri ili kupata Elimu itakayo saidia sekta ya mawasiliano sayansi na teknolojia katika nchi yetu"alisema Dkt .Turuka

Kwa upande wake Meneja  Mawasiliano wa Tcra Bw. Inocent Mungi aliwaasa wanafunzi hao kuwa kwenda kutumia fursa waliyoipata vizuri na siyo kusikia wanashiriki katika migomo.

"Jambo jema kwenda kufuata sheria za vyuo  na siyo vinginevyo na kwakufanya hivyo mtakuza talaamu yenu na kuwa watalamu wazuri ambao mtalisaidia nchi yenu katika sekta ya mawasiliano"alisema Bw. Mungi

Mmoja kati ya wanafunzi nane waliopata ufadhili huo Zaituni Kaijage alisema kuwa wahakikisha wanafanya vizuri ilikuweza kukabiliana na changamoto zinazolikumba Taifa hasa katia nyanja ya mawasiliano nchini, na kuomba sekta nyingine kuiga mfano huo wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.






No comments:

Post a Comment