Na David John
SHIRIKA la Ushawishi na Utetezi wa Haki za mtoto Tanzania (SUUHAMTA)liliko Chanika Ilala Dar es salaam limetoa msaada wa Unifomu , mabegi ya shule , viatu , soksi , vyenye thamani ya sh.552,000 kwa watoto 52 wanaoishi katika mazingira magumu ndani ya kata ya Chanika .
Akizungumzia msaada huo Dar es salaam juzi Mkurugenzi wa Shirika hilo ambalo liko chini ya ufadhili wa CRWRC Bw. Emanuel Msinga alisema shirika lake mbali na kufanya kazi ya kutetea haki za mtoto lakini pia hufanya kazi ya kulea watoto hao ikiwa pamoja na kuwapa mahitaji muhimu.
Alisema kuwa katika kituo,chao wanajumla ya watoto 93 na kati yao 52 wanatakiwa kwenda shule na kwa kutambua hilo shirika limeweza kutoa msaada huo ili waweze kwenda shule kama wezao.
"Nchi yetu inakabiliwa na changamoto la wimbi la watoto yatima ,wasiojiweza ,na wanaoishi katika mazingara magumu na serikalia inajitahidi katika kusaidia lakini bado kunahaja ya kuingozea nguvu ili kuweza kupunguza tastizo hili"alisema Bw.Msinga
Bw. Msinga alisema mbali nakutoa msaada huo kwa watoto hao lakini kama shirika wanakabiliwa na changamoto eneo ili waweze kujenga kituo kikubwa kitakacvhokuwa na uwezo wa kuchukua watoto wengi zaidi.
Naye Diwani wa kata hiyo Bw. Abdal Mpate alipongeza jitihada za shirika hilo hasa katika kuisaidia serikali kupambambana na wimbi hilom la watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini.
Alisema kuwa kwakutambua jitihada zinazofanywa na shirika hilo serikali ya kata Chanika itafanya jitihada za kuwatafutia eneo ili waweze kuwa na kituo kikubwa cha kulelea watoto hao.
"kwakweli kazi mnayofanya ni kubwa sisi kama serikali tutafanya jitihada za kuona namna gani ya kuweza kusaidia jambo hili ili muweze kuwa na eneo kubwa"alisema Bw. Mpate
Aliongeza kuwa katika kupambana na ongezeko la watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi ni vema wadau mbalimbali wazidi kujitokeza katika kuisaidia serikakali ili ifikie mahali kuweza kumaliza tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment