Na Mwali Ibrahim
BARAZA la sanaa Tanzania (BASATA) jana limezindua rasmi Taasis ya Tanzania Sana Faundation (TASAFO) itakayokuwa ikisimamia kazi za wasanii katika kuhakikisha wanapata kipato kinacholingana na kazi zao.
Akizindua rasmi tasisi hiyo kwa niaba Katibu Mkuu wa BASATA Gonche Matelego, Ofisa Sana Mtendaji wa BASATA Malimi Mashili alisema, kuwa BASATA imeridhia na madhumuni ya TASAFO na wapo tayari kushirikiana nao na cha msingi wazingatie haki za wasanii na sio kuangalia kujinufaisha wenyewe.
"Fanyeni kazi kama madhumuni ya taasisi na sio kuangalia manufaa yenu tu na jua nilazima mfanye kitu ambacho hata nyie kitawanufaisha lakini msiwe chanzo cha kuwanyonya wasanii," alisema.
Naye kwa upande wake Katibu wa TASAFO Shekha Said alisema, taasisi hiyo itakuwa ikisimamia wasanii waote bila kubagua aina ya kazi anayoifanya ikiwa ni kwa lengo la kumsaidia kupata kipato chake kiuhalali.
Alisema, wao watakuwa wakizinunua kazi zao na kuziuza huku wakiwapa wasanii kiasi chao walichokubaliana ikiwa ni pamoja na kuwatafutia masoko nje na ndani ya nchi.
Pia katika kufanikisha hayo watajenga kijiji cha sana kiitwacho Win to Win studio ambacho kitatumiwa na wasanii wakati wa kuandaa kazi zao ziwe za utamaduni, muziki au uigizaji.
Aliongeza kuwa pia watakuwa wakitoa mafunzo kwa wasanii kuhusu mila na tamaduni za makabila mbalimbali ili waweze kufahamu mila na tamaduni zao ili iweze kuwarahisishia katika utendaji wakazi.
"TASAFO katika kufanya kazi zake pia itakuwa ikiangalia pia mila na tamaduni za kitanzania ili kuhakikisha hata wasanii wake wanapata elimu kuhusu mambo hayo ambapo tayari tumeisha kutana na wasanii mbalimbali katika kulizungumzia hili na wamekubali," alisema.
No comments:
Post a Comment