01 February 2012

Maswali Bungeni

Na Peter Mwenda

Mbunge Martha Mlata aliuliza swali kuwa tatizo la upungufu wa madawati utakwisha lini?Jibu la Wizara ya Fedha ni kuwa fedha zilizotengwa kumaliza upungufu huo ni sh. bil. 18.4.

Swali la nyongeza kutoka kwa Bw. George Simbachewene aliuliza kuwa suala la upungufu wa madawati CCM ilichukulia ufumbuzi ulionesha tija kubwa , kwa kuwa mipango ya kumaliza ni halmashauri zetu Serikali Kuu inasema nini kuhusu suala zima la kumaliza upungufu wa madawati?

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI,) Bw. George Mkuchika anasema ni kweli shule za sekondari na msingi zina uhaba wa madawati, Tamisemi mwaka huu imeandaa waraka Waziri Mkuu atapeleke katika halmashauri zote kuwa huu ni mwaka wa kumaliza matatizo hilo.

Shule za msingi ni mali ya Serikali kijiji, shule za Kata ni mali ya Kamati za Maendeleo ya Kata hatuwezi kufanikiwa bila kushirikisha wananchi, tushirikiane kutoa michango ili kujenga kuziba pengo la Serikali.

Mbunge Bi. Amina Nasoro Makilagi aliuliza Je? Serikali imejipangaje kuwahakikisha  kuwa wanawake wanapata nafasi ya kutoa maoni yao?

Waziri wa Utawala Bora Bw. Mathiasa Chikawe anajibu kuwa tangu uhuru wa Tanzania Bara mwaka 1961,  Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuwakomboa mwanamke na mtoto.

Anasema Tanzania iliridhia mikataba ya kimataifa ya kumtetea mwanamke , Katiba ya 1977 sehemu ya Ibara ya 67 B inatoa nafasi ya wanawake na mtoto kulindwa.

Anasema wananchi wote bila kujali jinsia, rangi mwili au uwezo wa kifedha atapewa nafasi wa kutoa maoni yake.

"Kila mtu anao uwezo wa kufanya mawasiliano na kufanya masuala muhimu kwa jamii na wataelimishwa kwa kuandaa mikutano ya hadhara na vipeperushi.

Mtu yeyote atakayewazuia watakuwa wametenda makosa ya jinai watachukuliwa hatua za kisheria.

Makundi ya wanawake na wengine ambao hawawezi kutoa maoni yao mbele ya umati wa watu watatafutiwa njia nyingine kutoa maoni yao.

Mbunge wa Viti Maalum Dodoma, Bi. Bura aliuliza kuwa Serikali inatawachukulia hatuia gani wanaoportosha wananchi kutoa maoni yao.


Alisema wabunge wakianza kuelimisha wananchi wake na watu kuonekana wanaendelea kupotosha watachukuliwa hatua, Wizara inandaa vipeperushi na kuchapa katiba ya sasa kwa wingi na kusambazwa kwa wananchi.

Serikali imejipanga kuelimisha umma katika vyombo vya habari ya magazeti, redio na TV, Kuchapa nakala 500,000 za sasa na kuzisambaza kwa wananchi.

Serikali inandaa utaratibu wa kuchapa katiba mpya na tume itaweka utaratibu ili iwe sehemu ya mjadala.

Mbunge Ritha Mlaki anauliza kuwa Serikali za mtaa zinashindwa kuwaratibu watoto wa mitaani, Je ? Serikali itatusaidiaje kupia NGOS kupata idadi halisi ya watoto wa mitaani.

Jibu; Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto inasema kuwa katika halmashauri mbalimbali idadi halisi ya watoto inajulikana na kuomba asasi nyingine wengine wajitokeze.

Mbunge wa Igunga, Dkt. Kafumu Dalali nauliza kuwa asilimia 80 ya ya ardhi ya Igunga ni sehemu kame kwanini Serikali isijenge mabwawa ya kuvuna maji?.

Naibu Waziri wa Maji Bw. Jerry Lwenge anajibu kuwa Halmashauri ya Igunga imeteua  vijiji kumi ambavyo vitachimbiwa visima kati ya hivyo vinne vitaanza kuchimbiwa visima.

Hivyo Wizara hiyo inakubaliana na ushauri kuwa maeneo ambayo hayana maji ardhini wajengewe mabwawa.

Dkt. Dalali Swali ni mikakati gani serikali inayo ya kufikisha maji kutoka ziwa viCtoria utafanyika?


Naibu waziri wa Maji, Bw. Lwenge anasema Serikali imeanza mchakato wa kupeleka maji Tabora, Nzega na Igunga kutoka maji ya Ziwa Victoria.

Mbunge wa Rombo, Bw. Joseph Selasini aliuliza Je?  Wizara ya Maji iko tayari kutoa ruhusa fedha zilizotolewa kwa ajili ya kuchimba visima vitumike kujenga marambo?

Naibu Waziri wa Maji, Bw. Lwenge anasema ni kweli baadhi ya maeneo kumeshindikana kupata maji, wananchi pamoja na msimamizi waamue badala ya kuchimba visima wajenge mabwawa.

















No comments:

Post a Comment