LONDON,Uingereza
MSHAMBULIAJI Lusi Suarez amesema kuwa hatamwomba radhi Patrice Evra kutokana na mkasa wa kudaiwa alimtolea maneno ya kibaguzi.
Nyota huyo wa Liverpool alifungiwa mechi nane baada ya Chama cha Soka Uingereza kumkuta na hatia ya kumtolea maneno ya ubaguzi mchezaji wa Manchester United, Evra.
Lakini kwa mujibu wa The Sun, Suarez ambaye timu yake itapambana na United katika uwanja wa Old Trafford anasema ugomvi ubakie uwanjani.
Alisema: "Sikuwa na mawazo hata kidogo. Ninajua nilichofanya na aina ya sheria za soka ambayo inasema kitu kinachotokea uwanjani kinabakia uwanjani na huo ni mwisho wa stori."
Suarez, alikaririwa na Radio Sport 890 nchini Uruguay, akisema: "Ninajua dhidi ya Man United kutakuwa na wasiwasi kwakuwa nitakutana na Evra na kuongeza;
"Lakini kumekuwa na mashabiki wanaonipigia miluzi. Sidhani kama kutakuwa na kitu ambacho si cha kawaida kitatokea. Nitasahau kitu kilichotokea kwa wakati huo," alisema.
"Ninajua mashabiki wa Man United watajaribu kunifanya mimi nisijisikie raha.
"Lakini ninatakiwa kuwaeleza watanitia hamasa kama watanipigia miluzi."
Wakati huohuo, kuna habari kuwa klabu ya Liverpool inataka kumsaini kiungo wa Barcelona, Seydou Keita katika msimu ujao.
Mchezaji huyo anayedaiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 2 mwenye miaka 32, yuko na timu yake ya taifa ya Mali kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, amekuwa akiwekwa benchi na timu hiyo.
Keita anajua kuwa Liverpool inamtaka na atataka kuzungumza na kocha wa Barca,Pep Guardiola.

No comments:
Post a Comment