Na Zahoro Mlanzi
MECHI ya Ligi Kuu Bara kati ya timu ya Simba na Azam FC, iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,548,000.
Mchezo huo ulipigwa juzi kwenye uwanja huo ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, mabao yote yalifungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema
watazamaji 19,257 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 117 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa viti maalum (VIP) A.
Alisema baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 10,303,932.20 kila timu ilipata sh. 13,182,800.34, uwanja sh. 4,394,266.78.
"Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimepata sh. 1,757,706.78, TFF sh. 4,394,266.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,197,133.39, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 439,426.78 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,394,266.78," ilieleza taarifa hiyo.
Alisema gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000 na wamuzi wa akiba sh. 30,000.
Pia alisema gharama za tiketi ni sh. 4,350,000, maandalizi ya uwanja sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina walipata sh. 2,000,000.
Alisema pamoja na gharama hizo pia kuna gharama nyingine za Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi ambapo kila klabu ilipata sh. 1,347,990,280 wakati DRFA ilipata sh. 1,555,420.
No comments:
Post a Comment