Na Peter Mwenda, Mkuranga
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), umetoa ofa nyingine kwa wanamichezo watakaojitokeza kununua nyumba tatu zilizobaki ambapo watauza kwa sh. mil. 9.5 kila mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati walipokwenda kutembelea nyumba tano zilizojengwa na wasanii hao, Mwenyekiti wa mtandao huo, Cassim Taalib alisema ofa hiyo ni moja ya mikakati ya kutafuta fedha za kujenga nyumba 1,000 za wasanii.
Alisema SHIWATA inatarajia kufanya matamasha
makubwa nchini kutafuta fedha kwa ajili ya
ujenzi huo ikiamini kuwa wasanii wengi huishi maisha ya kimasikini baada ya kustaafu kazi za sanaa na wengine kukosa mahali pa kuishi kwa vile vipato vyao havina uhakika kwa kuandaa sehemu ya makazi.
"Sisi wasanii tunao uwezo wa kucheza filamu,
kcheza soka, kuigiza na kazi nyingine za sanaa, ngoma na nyingine ambazo zinaweza
kuingiza fedha za kuchangia wasanii ambao
hawana uwezo kabisa wa kujenga" alisema Taalib.
Taalib alisema katika nyumba tano za awali
ambazo zimekamilika zimejengwa kwa njia ya
kujichangisha kila mmoja na SHIWATA ilitoa ofa ya punguzo la sh. 1,250,000 kwa wanachama watakaokamilisha mchango wa sh.3,250,000 kati ya Septemba 10, 2011 na Desemba 31, 2011.
Alisema wanachama wawili, Josephine Mushi ambaye ni mwandishi wa habari na Flora Kafwembe ambaye ni Msanii wa Kikundi cha JKT waliibuka washindi baada ya kukamilisha michango yao kwa wakati.
Taalib alisema ujenzi wa nyumba hizo na
nyingine zote zitajengwa kwa mfumo huo huo wa tofali za saruji na matofali ya kupachika.
Alisema Ujenzi wa nyumba tano za awali
umegharimu sh. mil. 33,000,000 na wanachama 180 walianza kuchangia ujenzi.
No comments:
Post a Comment