02 February 2012

SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa nchini (BFT) limesema hatma ya Tanzania kupata mabondia

Wazuri watakaoweza kufuzu michuano ya Olimpiki itajulikana katika mashindano ya majiji yatakayofanyika Nairobi Kenya, Februari 26 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe alisema mashindano hayo ndiyo yatakayotoa majibu ni mabondia wepi watakaokwenda Casablanka kusaka viwango vya Olimpiki.

Alisema katika mashindano hayo Tanzania itawakilishwa na mabondia kutoka jiji la Dar es Salaam na Mwanza kutokana na michuano hiyo kushirikisha majiji.

Alisema uwezo wa mabondia utaonekana katika mashindano hayo kutokana na kushirikisha mabondia wengi wazuri kutoka katika nchi mbalimbali Afrika.

"Mabondia wote wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati watasaka viwango vyao vya kucheza Olimpiki nchini Casablanka hivyo vipimo vya mabondia wetu ni wepio waende na wepi wabaki hatma yake itajulikana katika michuano ya Majiji,"alisema Changarawe.

Mabondia wa Tanzania kwa sasa wanaendelea kujifua kujiandaa na michuano hiyo ya kufuzu Olimpiki ambapo BFT imeandaa mashindano ya mchujo kwa ajili ya kupata mabondia wenye viwango vizuri.

No comments:

Post a Comment