03 February 2012

Serikali kuimarisha midahalo ya kijamii

Na Goodluck Hongo

Serikali imesema itaendelea kuimarisha midahalo katika ngazi zote za jamii ili kuwafanya wananchi kushiriki  juu ya mambo ya Taifa

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa tatu wa kila mwaka wa majadiliano ya kisera baina ya wadau wa maendeleo na serikali Waziri wa Fedha Bw.Mustafa Mkulo alisema kutokana na majadiliano hayo ujumbe umepatika

"Katika majadiliano haya ya siku mbili ujumbe umepatikana (key messages) na Serikali itaendelea kuimarisha majadiliano hayo katika kila ngazi ya jamii ili kushiriki katika mambo ya Taifa

Alisema Serikali na la kila mmoja wetu hapa tunahitaji kuchukua hatua ili tusonge mbele huku tkukirekebisha sera zetu,mipango ya kukua,maendeleo na kupunguza umaskini

Akizungumza siku ya kwanza ya majadiliano hayo Mwenyekiti Mwenza wa Kundi la Washirika wa Maendeleo na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw.Alberic Kacou alisema  Tanzania imejiimarisha kwenye maendeleo ya watu

"Jambo linalostahili kutambuliwa katika majadiliano haya ni kwamba Tanzania imekuwa na mwelekeo chanya wa ukuaji katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika kuimarisha utendaji wake kwenye maendeleo ya watu" alisema

Alisema Tanzania kwa kulinganisha na  nchi nyingine,inaendelea kubaki kuwa ndio nchi inayofanya vema sana katika ukanda kusini mwa jangwa la sahara

Alisema licha ya maendeleo ya kutia moyo bado kuna changamoto za kutosha zinazohusiana na kupunguza umasikini ambapo wataznania asilimia 65 wanaishi katika umasikini wa pande nyingi

Alisema huku wakiwa na fursa chache za elimu,afya,maji salama na safi,usafi.umeme,nishati ya kupikia na mali ni muhimu kwa Serikali na Washirika wake wa Maendeleo wafanye juhudi zaidi kwenye viwango vya kupungua umasikini

Kwa upande wa sekta binafsi wao wameishauri Serikali kuwekeza zaidi katika miundombinu ya reli na bandari ikiwemo umeme ambapo waliiomba Serikali kuwa na mipango ya muda mrefu ya upatikanaji wa umeme na sio muda mfupi

Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda na ulihudhuriwa na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanadiplomasia, Wakuu wa Mikoa, wawakilishi wa asasi za kiraia, Wabunge, Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wakilishi wa sekta binafsi     


No comments:

Post a Comment