Kuhusu nyongeza ya posho za wabunge kuwa ni ya kinafiki na haionyeshi uongozi thabiti na inalenga kujisafisha kwa wananchi dhidi ya viongozi waandamizi wa chama na wabunge wake kutaka nyongeza ya posho kinyemela.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Bw. John Mnyika, kauli hiyo ni muendelezo wa kauli za CCM za kujikosha mbele ya umma baada ya wananchi kupinga maamuzi ya serikali.
Alisema kauli kwamba ‘CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na mchakato wa nyongeza ya posho za vikao kuliangalia upya na kutumia busara na ikiwezekana kuachana nalo kwasasa inadhihirisha kwamba chama hicho kimepoteza uwezo wa kuwa chama tawala.
Alisema kauli zinazotolewa na CCM zinadhihirisha ulegelege wa chama na serikali yake katika kusimamia masuala ya msingi na ya taifa hali ambayo athari zake zinathibitika hivi sasa katika mjadala huu wa posho ambapo ombwe na uongozi linaonekana bayana katika chama hicho na serikali.
Alisema kumpongeza Rais Kikwete kwa kushindwa kuonyesha uongozi na badala yake kutupa mzigo wa wabunge kwenye suala ambalo kwa mujibu wa sheria Rais ndiyo mwenye mamlaka nalo ni ishara ya CCM kulea viongozi wasiowajibika miongoni mwa viongozi wakuu wa serikali na chama hicho.
Aliongeza iwapo CCM ingekuwa na dhamira ya kweli ya kukataa posho za vikao ingefanya hivyo kupitia vikao vya chama hicho vya kamati kuu na halmashauri kuu ambavyo viliongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete wakati ambapo mjadala wa posho za vikao ukiwa tayari umekolea katika taifa.
Aidha CHADEMA inaitaka CCM kama kweli inajali maslahi ya wananchi kufanya maamuzi ndani ya vikao na kuandaa mapendekezo kwa serikali ya kufuta posho zote za kwenye mfumo wa utumishi wa umma kama ilivyoelezwa katika ilani ya CHADEMA.
Pia CCM itoe mwito kwa Rais Kikwete kufuta posho hizo katika mfumo wa utumishi wa umma na kutoa kauli ya wazi ya kukataa nyongeza ya posho za wabunge.
Aliitaka CCM kueleza ni hatua gani inawachukulia wanachama walionukuliwa kwenye vyombo vya habari wakisema kwamba Rais Kikwete amebariki nyongeza ya posho na hivyo kukosekana kwa uwajibikaji wa pamoja katika serikali na chama hicho.
Alisema CHADEMA inaendelea kusisitiza kauli yake kwamba ongezeko la posho ya vikao
lilofanyika linapaswa kusitishwa kwa kuwa limefanyika kinyume na taratibu na pia halina uhalali kimantiki na halijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla; nyongeza hiyo ya posho ni haramu.
Aliongeza kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge ya mwaka 2008 kinataja aina ya posho ambazo wabunge wanastahili kulipwa niusafiri, kujikimu na wasaidizi na katika orodha hiyo hakuna posho ya vikao.
Alisema kupungua kwa uzalishaji, kiwango cha fedha pamoja na kuongezeka kwa ubadhirifu katika matumizi ya rasilimali za umma kunachangia mfumuko wa bei hali inayohitaji mpango wa dharura wa kunusuru uchumi.
No comments:
Post a Comment