03 February 2012

SERIKALI inapata hasara kubwa hususani katika sekta ya ardhi

Kutokana na wapima ardhi kutotambuliwa na wananchi pamoja na kutopewa kipaumbele serikalini.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam juzi na Muelekezi Mkuu  kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) Bw. Ambogo Ambogo wakati alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano mkuu wa wapima ardhi.

Bw. Ambogo, alisema kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana  bila ya uwepo wa wapima ardhi.

Aliongeza kuwa endapo wapima ardhi wakitumika vyema kusingekuwa na matatizo ya watu kukumbwa na mafuriko, migogoro ya ardhi pamoja na maghorofa kuangaku ovyo ovyo kwa kuwa wao waneweza  kujua viwango bora vya ardhi.

Alisema kuwa serikali imekuwa ikipata hasara kutokana na kutowatumia wataalamu wa kupima ardhi hivyo wanaweza kutumia fedha nyingi kwa kuwatumia watu ambao si wataalamu.

Akizungumzia changamoto katika taaluma hiyo kwa upande wa elimu na mafunzo alisema kuwa serikali inashindwa kuwekeza kwa wapima ardhi kutokana na gharama kubwa kutokana na tatizo la uchumi.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni wanafunzi kukimbia masomo ya hesabu na fizikia, uhaba wa vyuo vinavyotoa shahada ambapo kwa sasa nchini  kipo chuo kimoja tu ambacho ni Chuo cha Ardhi pamoja na uelewa wa lugha ya kufundishia kwa wanafunzi ambapo asilimia kubwa wanafunzi wanakalili tu.

"Lugha ya kufundishia pia ni tatizo kwani wanafunzi wengi wana kalili tu kutokana na kutoelewa kile wanachofundishwa hivyo ni vyema kiswahili kingetumika", alisema Bw. Ambogo.

Kwa upande weke Katibu wa Halmashauri ya Bodi ya kusajili wapima ardhi Bw. Nassor Duduma, alisema kuwa matatizo ya ardhi ni mengi na kukitaka Chama cha  Wapima Ardhi Tanzania(IST) kijitangaze kwa wananchi ili waweze kufahamu ni wapi wanaweza kuepukana na matatatizo ya ardhi.

Alisema kuwa ni vyema chana hicho kikaandaa utaratibu wa kufungua milango kwa kusikiliza kero za wananchi ili kuwaelimisha waweze kuelewa umuhimu wa wapima ardhi.

Alisema kuwa kutokuwepo kwa kitengo au sehemu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa wapima ardhi ni tatizo linalosababisha kuwepo kwa migogoro hiyo kila kukicha.

Katika mkutano huo makampuni matatu kutoka China na Kenya  yalionyesha vifaa vya kisasa vya kupimia ardhi sambamba na kampuni zingine tatu za Tanzania.

No comments:

Post a Comment