03 February 2012

KUFUATIA kuendelea kwa mgomo wa madaktari nchini,

Madaktari hao wameombwa kurejea kwenye vituo vyao vya kazi na kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha uzalendo na taifa lao wakati serikali ikiendelea kushughulikia madai yao.

Wito huo kwa madaktari umetolewa Dar es Salaama jana na Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Nchini(TPN) Bw. Phares Magesa, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

"Ninachoomba madaktari warudi makazini wakati serikali ikiendelea kushughulikia madai yao, pia serikali iwashirikishe madaktari hatua gani zinachukuliwa katika kutekeleza madai yao," alisema.

Bw. Magesa, pia aliitaka serikali iharakishe mazungumzo na madaktari na itoe ahadi ya kutekeleza madai ya madaktari kadri uwezo utakavyoruhusu.

Pia aliitaka serikali ifikirie upya uamuzi wake wa awali wa kuwafukuza kazi wale madaktari ambao walikuwa bado hawajaripoti kazini kama agizo la Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.

Alisema kuwa ni virui hatua nyingine za kinidhamu kikachukuliwa badala ya kuwafukuza kazi kwa sababu nchi ina upungufu mkubwa wa wataalamu katika sekta hiyo.

Pia aliwataka wale wotewaliotajwa katika taarifa mbalimbali kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwajibika kwa kutoa kauli zilizochochea au kukuza mgogoro huo waombe radhi na kama wakishindwa kufanya hivyo wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Bw. Magesa, aliwaomba watanzania, viongozi, watendaji wa Taasisi za Umma na binafsi kuwa waadilifu kwa kuzingatia dhana ya utawala na uongozi bora na kuwa wazalendo wa kweli na kuweka mbele utaifa na maslahi ya walio wengi.

Alisema kuwa suruhu ya matatizo sio migomo bali ni mazungumzo na kama serikali inaweza kutekeleza yale yanayotekelezeka yatekelezwe.

Hata hivyo aliwataka madaktari hao kuangalia uchumi wa nchi husika kwa kuwa mapato ya serikali kwa sasa hayawezi kukidhi matakwa ya sekta zote.

Mwisho


No comments:

Post a Comment