01 February 2012

MBUNGE wa jimbo la Kigamboni aitishia Serikali

Na Andrew Ignas.

MBUNGE wa jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Bw.Faustine Ndugulile ametishia kusitisha mradi wa Kigamboni kama serikali itashindwa kutoa majibu sahihi ndani ya  miezi minne.


Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili jana wakati wa Balaza la Madiwani lililofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Temeke, Mbunge huyo amesema kuwa anaipa serikali miezi minne tu ili watoe majibu sahihi kuusiana na hatima ya miradi wa kigamboni ambao unaoneakana kuchangia kupungua kwa shughuli za maendeleo.

'Kutokana na kero ambazo zinawakumba wananchi wa jimbo langu kwa kushindwa kuendeleza nyumba zao,kupanua ujenzi wa shule na huduma nyingine mbali mbali sitaweza kulinyamazia hilo nitalazimika kusitisha mradi wao kama watashindwa kutoa maamuzi ya kina ndani ya miezi minne ambayo itakuwa juni 30 mwaka huu"alisema Ndugulile.

Wakati huo huo Mbunge huyo amesema amepanga kukutana na Waziri Mkuu Bw.Mizengo Pinda wajadili kwa kina ongezeko la Kivuko.

"Nimemtumia Waziri Mkuu ujumbe ili tuzungumzie ongezeko la Kivuko kwa wananchi ambao wapo katika wakati mgumu kutokana na wengi miradi yao ku kwama  kwa kuso mikopo ambayo usababishwa kutokuwa na  Hati na aseti za kutoamishika zikiwemo nyumba"alisema huyo.

Hata hivyo imeiomba serikali kutumia hekima,busara na kutazama njia mbadala za kusghulikia tatizo la mgomo wa Madaktari unaoendelea hivi sasa.

Aidha kwa upande mwingine Mstahiki meya wa Halmasahauri ya Temeke Maabadi Suleimani Hoja umeahidi kuboresha  miundo mbinu mbali mbali ya idara ya afya ikiwemo nyongeza ya mishahara na ununuzi wa Madawa pamoja na vitendea kazi.

Pia Balaza la Madiwani wa Halmsahauri hiyo limewapongeza Madaktari baada ya kuendelea ba kazi badala ya kugoma sambamba na kumtaka  Mkurugenzi wa Temeke Bi Marghareth Nyalile kukutana na Bodi ya afya ya Mkoa huo ili wajadili kero zinazo ikabili idara hiyo na kulifanyia kazi.





No comments:

Post a Comment