06 February 2012

Mbishi Real: Msanii anayelia na ubakaji

FRED Kaguo ‘Mbishi Real’ ni miongoni mwa wasanii wanaolia na wasanii wanaotumia ambazo kwa upande mwingine zinawaangamiza na vipaji vyao kuishia pasipojulikana.

Tunawaona wasanii mbalimbali wazuri na wenye majina makubwa wakiangamia kila siku kwa kutumia madawa ya kulevya.

Na wengi wao hujiingiza katika utumiaji wa madawa kama masihara na baadaye wanakuwa watumiaji wa kupindukia na kusahau kazi zao.

Mbishi Real, anatamba na vibao vingi ukiwemo 'Tozi Wa Mbagala'
uliomtambulisha vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya na kutawala katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mitaa kadhaa ya Dar es Salaam, wimbo huo umekuwa gumzo kutokana na ubunifu wa washiriki katika video ya wimbo huo na
kusababisha vijana wengi kuigiza miondoko hiyo na kubandika plasta shavuni.

Mbishi real, alianza shughuli za muziki jijini Mbeya miaka kadhaa iliyopita akiiga mashairi mbalimbali ya wasanii wakongwe  waliokuwa wakiwika kwa nyakati hizo.

Anasema katika kazi zake aliweza kushirikiana vyema na wasanii
mbalimbali akiwemo marehemu Comprex katika kibao chake cha Business.

Alishirikiana na wasanii wengine kama Chege, Jay Mo katika kibao kinachojulikana kama 'Amebaka', kinachofanya vizuri
katika vituo mbalimbali vya redio.

Anasema, lengo la kuwashirikisha wasanii wengi katika nyimbo zake ni kujenga uhusiano mzuri katika tasnia ya muziki huo ili kuupeleka muziki wao kimataifa zaidi.

Mbishi Real anasema, anakubalika zaidi kutokana na nyimbo zake kuwa ni sehemu ya mafunzo kwa jamii bila ya kujali rika na  maisha halisi ya Mtanzania.

"Nyimbo zangu ukizisikiliza ni kwa ajili ya kutoa mafunzo mbalimbali kwa jamii kutokana na maudhui yenyewe, mfano wimbo wa 'Amebaka', ni matendo ambayo kila kukicha yamekuwa yakitokea katika jamii na kuathiri  jamii nyingi” anasema.

“Nimeona nikitumia mashairi inawezekana baadhi ya watu walio na tabia hiyo wanaweza kuacha kutokana na athari nyingi
zinazopatikana ikiwemo kuongezeka kwa mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.

“Hivyo jamii ikielimika, suala la ubakaji linaweza kupungua, na wakati mwingine hali inakuwa mbaya kutokana na watoto wadogo zaidi, wengine wakiwa na umri wa miaka mitatu ambao  hajajua lolote wanafanyiwa vitendo hivyo,” anasema Mbishi Real.

Anasema, katika moja ya nyimbo zake ameweza pia kuzungumzia haki za watoto kawa ujumla wao ambao kwa njia moja au nyingine wamakuwa wakizikosa.

Anasema, kutokana na kutaka kulitawanya soko lake kimuziki na kukonga nyoyo za mashabiki wake, anaimba nyimbo katika
mahadhi yote ili kila shabiki apate ujumbe na burudani kwa mpigo.

Msanii huyo mwenye elimu ya kidato cha sita, anawaomba  wasanii wenzake kujiendeleza kielimu kutokana na kuamini kuwa muziki bila elimu ni sawa na kujenga nyumba bila ya msingi.

“Elimu ni kila kitu katika maisha, hivyo ni vyema wasanii wakajifunza zaidi muziki kwa kwenda darasani ili kuufahamu zaidi
na shule ya kujiendeleza katika fani nyingine ni muhimu kutokana
na maisha ya sasa ambayo wakati mwingine ni vigumu kuyatabiri,” alisema Mbishi Real.

Baadhi ya nyimbo zilizokuwemo katika albamu yake kwanza  inayotarajiwa kutoka baada ya mfungo wa Ramadhani kuisha ni pamoja na nyimbo yake ya kwanza ya Business, aliyomshirikisha
marehemu Complex, 'Pombe' aliomshirikisha Q Jay na
'Nimesomeka' alioimba na Bwana Misosi, Tozi Wa Mbagala na
'Amebaka' aliomshirisha Chege pamoja na Jay Mo.


No comments:

Post a Comment