01 February 2012

Matumizi ya dola yanachangia mfumuko wa bei


Na Rose Itono

IMEELEZWA kuwa matumizi ya dola ndani ya nchi yanachangia mfumuko wa bei  hali inayochangia maisha  ngumu na wananchi kushindwa kusonga mbele


Hayo yalisemwa Dar es Salamam juzi na wadau wa semina za Jinsia (GDSS) walipokuwa wakijadili athari zinazowakumba wanawake na makundi yaliyoo pembezoni kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania,mfumuko wa bei na hali ngumu ya maisha.

Bw. Badi Darusi mdau wa (GDSS) alisema kuwa ununuzi wa bidhaa zetu kwa kutumia dola kunachangia sana kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

Alisema sasa hivi shule nyingi yamekuwa yakipenda malipo ya ada yafanywe kwa kutumia dola, kutokana na kushuka kwa thamani hivyo kuendelea kukubaliana na hali hiyo tutaendelea kufanya sarafu yetu kushuka thamani na kushuka kwa uchumi.

Alisema pamoja na uchumi wa nchi kutetereka bado kuna nafasi kwa viongozi wetu kusimama imara kukabiliana na hali ngumu ya uchumi kwa kufufua viwanda vyetu ili viweze kuzalisha.

Bw. Darusi alisema enzi za baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kulikuwa na viwanda visivyopungua 582 ambapo mikoa mingi ilikuwa ikijitegemea kwa shughuli za uchumi.

"Shughuli za kilimo na viwanda ziliendelea kuendeshwa katika mikoa hiyo bila tatizo hali iliyosaidia kukuza uchumi wa nchi,"alisema Bw.Darusi.

Aidha aliongeza kuwa,Mfumo wa soko huria unaosimamiwa na Shirika la Ubinafsishaji (PSRC) ulichangia kwa kiasi kikubwa viwanda vingi kuanza kuporomoka.

Hali hii ilitokana na serikali kushindwa kudhibiti mfumo wa bei ambao umeathiri jamii kubwa na kusababisha uwepo wa matabaka ya walionacho na wasionacho.

Alisema hali hii imeathiri sana maisha katika ngazi ya kijamii na kifamilia kutokana na kushuka kwa uchumi ambapo jamii kubwa imekuwa ikishindwa kumudu gharama za maisha na kuitaka serikali kudhibiti mfumo huo.


2 comments:

  1. Tatizo kubwa BOT na Treasury vinaendeshwa kama miradi ya wanasiasa. Sasa hivi kuna juhudi zinafanyika eti mawaziri ndio wawe accounting officers. Wanagawa pesa kama njugu. Haingii kwenye akili serikali kuuza kiwanja kwa sh20000 per square meter hizo pesa zinapopatikana zinaingia kwenye mifuko ya mafisadi na wao kuzigawa hovyo. Dawa ccm itoke madarakani tupate new thinking

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wekeni namba ya dawati la makala, tunataka kuuliza mengi kuhusu jinsi ya kuandika makala katika gazeti lako.

      Pia tuna barua za wasomaji tutapataje?

      Delete