Na Tumaini Maduhu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Airtel kupitia huduma ya Airtel Money imefanikiwa kupata miji zaidi ya themanini ambayo inatumia mtandao wa Airtel Money kwa ajili ya huduma za pesa.
Akizungumza wakati ya semina ya huduma ya Airtel money kwa wadau na sekta mbalimbali wakiwemo wadau wa usafirishaji, asasi za kifedha, wakuu wa shule na vyuo vya elimu ya juu Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni hiyo Bi. Beatrice Mallya alisema utafiti unaonesha huduma hiyo imekubalika kwa wateja.
Alisema, kuwa wamefanikiwa kuvuka kiwango hicho kutokana na huduma hiyo kuwa rahisi na yenye ubora katika kutoa pesa na kuingiza ukiwa mahali popote nchini.
Alisema kuwa licha, yakufanikiwa kupata miji hiyo pia Airtel ina mpango mkakati wakuhakikisha inaboresha huduma za kijamii nakuiboresha huduma ya Airtel Money kuwa yenye ubora kwa Watanzania.
"Tunashukuru hapa,tuliofika kwasababu juhudi na matunda yanayoenekana kutokana na kupata wateja zaidi ya elfu kumi na kupata miji themanini kutokana na kuenea karibu maeneo yote nchini,"alisema
Alisema waligundua huduma hiyo ni nyenzo muhimu katika kuweka urahisi usalama zaidi pamoja na kupunguza hatari zinazotokana na kutembea na fedha nyingi au kukaa ofisini na fedha nyingi kwa lengo la kuzitumia katika shughuli za wiki nzima au kulipa mahitaji mbalimbali.
"Airtel Money ni suluhisho la kufanya hayo yote na ndio maana leo hii tumekaa pamoja kwa lengo la kuweka kila kitu bayana kwa wadau hawa muhimu kwetu,"alisema
Akitoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel Money ambapo kwa kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kulipa Ankra kama vile ada ya shule, mishahara ya wafanyakazi au vibarua, kufanya makusanyo ya mauzo ya siku, kulipia huduma za DSTV, Luku, bili ya DAWASCO, kulipia visa ya USA, pamoja na kutuma na kupokea hela ndani na nje ya nchi.,
No comments:
Post a Comment