Na Tumaini Maduhu
KAMPINI ya simu za mkononi Airtel kupitia huduma ya Airtel Money imefanikiwa kupata miji zaidi ya themainini ambayo inatumia inatumia mtandao wa Airtel Money kwaajili ya huduma za pesa.
Akizingumza na waandishi wa habari juu ya huduma ya Airtel Money Mkurugenzi wa mawasiliano Kampuni hiyo Bi Beatrice Mallya alisema, kuwa wamefanikiwa kuvuka kiwango hicho kutokana na huduma hiyo kuwa rahisi na yenye ubora katika kutoa pesa na kuingiza ukiwa mahali popote Nchini.
Alisema kuwa licha, yakufanikiwa kupata miji hiyo pia Airtel ina mpango mkakati wakuhakikisha inaboresha huduma za kijamii nakuiboresha huduma ya Airtel Money kuwa yenye ubora kwa watanzania.
``Tunashuru hapa, tuliofika kwasababu juhudi na matunda yanayoenekana kutokana na kupata wateja zaidi ya elfu kumi na kupata miji themanini kutokana na kuenea karibu maeneo yote Nchini``alisema,Bi Mallya.
Aliongeza Kampuni hiyo imefanikiwa kusogeza huduma za kijamii kwakutoa misaada mashuleni,huduma mahospitalini na promosheni mbalimbali zilizowainua watanzania wengi.
``Tunawaomba wateja wetu watumie mtandao huu kwasababu kupitia mtandao huu tumesogeza huduma za kijamii kwa Wananchi,na mashindano ambayo yamewakwamua watu wengi kwenye hali ngumu ya maisha``alisema ,Bi Mallya,
No comments:
Post a Comment