a Damiano Mkumbo, Singida
KIWANGO cha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida mkoani Singida kimeshuka kutoka sh. milioni 79.8 hadi kufikika sh. 58.6 katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka 2011.
Hayo yalibainishwa katika taarifa ya mapato iliyotolewa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kilichoketi kwenye ukumbi wa manispaa hiyo hivi karibuni.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa kushuka kwa kiwango hicho ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mdororo wa uchumi, baadhi ya wateja kutolipa kodi na ushuru unaotakiwa kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo ambayo inaonesha kusababisha halmashauri hiyo kushindwa kutekeleza utoaji wa huduma ipasavyo, vikosi kazi saba vyenye madiwani na watendaji vimeundwa ili kufuatilia mwenendo wa ukusanyaji na kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa miradi.
Madiwani wa mamlaka hiyo walisema, jambo hilo litawezesha kupata hali halisi ya makusanyo ya mapato kutoka vyanzo vya ndani na hivyo kuelewa vikwazo vilivyopo ili kupata ufumbuzi wake.
Walishauri vikosi kazi hivyo vifanye kazi kwa awamu tofauti na kupeleka taarifa zake katika kamati zinazohusika kabla ya kufikishwa kwenye Baraza la Madiwani hao katika kikao kijacho.
Akifunga kikao hicho Mstahiki Meya wa halmashauri hiyo, Bw. Salumu Mahami alizisisitiza umuhimu wa kuanza kwa zoezi hilo mwezi huu.
“Madiwani ndiyo nguvu kazi za halmashauri hii, wakishirikiana na watendaji, hivyo wahamasisheni wananchi kuwa ulipaji wa kodi na ushuru unaostahili kulipwa kwani ndiyo uhai wa mamlaka hii,” alisema
No comments:
Post a Comment